logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Siwezi kuoa mwanamke mwenye mtoto labda wafukue kaburi wapime mifupa ili niamini alikufa - Mr Mwanya

Mr Mwanya amefichua kiini ambacho humufanya kuimbaa miziki yake akiwachana wanadada ambao alitengana nao kwenye mahusiano

image
na Japheth Nyongesa

Burudani07 March 2025 - 12:01

Muhtasari


  • Mr mwanga kazi ambazo amezifanya kwa wingi zinahusisha kuwashambulia wanadada ambao aliachana nao kimahusiano ziwe za mziki au vichekesho.
  •  Amesisitiza kwamba yeye hawezi kumini kwamba 'baby baba" hana mahusiano na msichana yeyote hata kama ataoneshwa kaburi lake.

Mchekeshaji na mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Mr Mwanya amefichua kiini ambacho humufanya kuimbaa miziki yake akiwachana wanadada ambao alitengana nao kwenye mahusiano. Mchekeshaji huyo pia amekiri kwamba hawezi kuoa mwanamke mwenye mtoto.

Kwenye swala la kuwachana warembo ambao waliachana amesema  kwamba yeye huimba akituma ujumbe kwa ma ex huku akiwakilisha watu wote wenye lengo sawa.

Mr mwanga kazi ambazo amezifanya kwa wingi zinahusisha kuwashambulia wanadada ambao aliachana nao kimahusiano ziwe za mziki au vichekesho.

Kwenye mahojiano na mwanahabari alipoulizwa alikuwa na haya ya kuserma " Ex ni kisasi Vitu ambavyo alinisababishi kipindi ambacho tulikuwa kwenye mahusiano, na kwangu mwanzoni Ex nilimuchana mara mbili tu. lakini wakati nilikuwa nimeacha mashabiki zangu walitaka niendelee," alifichua mwanamziki huyo.

Kila mtu ana Ex wake, hata wewe una ex, kwa hivyo mashabiki zangu wanapenda vile mimi namshambulia. Wanalinganisha na maisha yao pia ya kila siku kwa hivyo huu ni mwendelezo nikaona niwape mashabiki wangu wanachokitaka.

Mwanga kwenye jambo la kuoa mwanamke ambaye ana mtoto ameesitiza kwamba yeye haamini kwamba mtu kaachana na mpenzi wake wakati walizaa pamoja. Amesisitiza kwamba yeye hawezi kumini kwamba 'baby baba" hana mahusiano na msichana yeyote hata kama ataoneshwa kaburi lake.

"Kuhusu wanadada ambao wako 'single' na wana watoto, mimi nimepatana nao. Ila mgogoro wangu mkubwa kwa masingle mother ni kwamba mimi binafsi msimamo wangu ni kwamba siwezi kuja kuoa mwanamke mwenye mtoto. hata kama nikioneshwa kaburi la baba mtoto siwezi. Labda lile kaburi wakishanionesha wafungue mifupa wapeleke kwenye labu wepime. mimi nina wivu wa kimapenzi," alieka wazi mchekeshaji huyo wa Tanzania


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved