
TIKTOKER Nyako aibuka tena kwenye mitandao huo baada ya ukimya wa takribani miezi minne, na safari hii ujio wake haujaja kwa kuchamba bali kwa unyenyekevu wa kuomba msaada.
Nyako ambaye alikuwa anajulikana kwa kutengeneza pesa nyingi
kupitia vipindi vya mubashara kwenye mitandao huo wa video fupi alifanya video
ya kutia huruma akiwalilia mashabiki wake kumsaidia na hela za kulipa kodi ya
nyumba.
Nyako alisema kwamba kwa sasa angependa kujikimu kivyake na
hataki hela za Wajerumani, akisema kwamba yuko tayari kupokea zawadi za TikTok
ambazo baadae hugeuzwa kuwa hela.
"Mimi ninaomba mnisaidie tu kulipa rent, nimekuwa nje ya TikTok miezi mitatu hadi minne na ninarudi, zawadi bado ninahitaji kwa sababu nimeamua kujikimu kivyangu kimaisha mimi sitaki pesa za wajerumani nimeamua kujikimu kivyangu kimaisha," Nyako alisema.
Bila kueleza sababu ya kutoonekana kwenye TikTok kwa muda wa
takribani siku 100, Nyako alisema kwamba sasa atarudi kwa kivumbi na kimbunga
cha kipekee, lakini akasisitiza kwamba hawezi kata msaada wa zawadi kutoka kwa
wafuasi wake.
"Hivyo mimi ninaomba
hapo mahali tuliachia tuendelee hapohapo tunaendelea kwanza wakati huu ninarudi
kwa njia ya kipekee kwa sababu vile mnajua tuko na jikoni kubwa, na nyumba ni
kubwa hivyo tunarudi kwa ukubwa wa kipekee, hakuna matusi nimechoka kwenda
kortini na watu na story ya kwenda kortini ilikua ikapiga kona ikaenda, sina
muda wa hilo," alisema.
Mara ya mwisho akifanya vipindi vya Live kwenye TikTok, Nyako
alidokeza kwamba alikuwa anapambana na tatizo la moyo, huku akiwatia wasiwasi
mashabiki wake kwa kujitabiria kifo kwamba asingeishi muda mrefu.