Taifa la Kenya linashikilia nafasi ya 115 katika watu wenye furaha duniani kulingana na utafiti wa hivi punde..Majirani wa Kenya Uganda
wanashikilia nafasi ya 116, Somalia ni ya 122. Finland imeorodheshwa kuwa nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mwaka wa nane mfululizo.
Wataalamu wanaamini kuwa ukaribu wa Wafinlandi na asili pamoja na upatikanaji wa mfumo mzuri wa ustawi husaidia kuelezea nafasi yake ya juu inayoendelea katika Ripoti ya Furaha ya Dunia inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.
Denmark ilikuja nafasi ya pili.
Costa Rica na Mexico zimekuwa miongoni mwa nchi kumi bora kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka kumi na tatu ya Ripoti hiyo , ambapo uhusiano mzuri wa familia ulitajwa kigezo muhimu.
Hata hivyo Tanzania imeibuka nafasi ya 136 dhidi ya mataifa 147 yaliyotathminiwa.
Hii ni kulingana na ripoti ya toleo la kumi na tatu la siku ya furaha duniani ambayo huadhimishwa Machi 20 kila mwaka.
Ripoti ya mwaka huu ilikuwa inaangazia jinsi watu wanavyojali wenzao na kushirikiana na kusema hilo linachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na furaha zaidi kuliko kuwa na mshahara mkubwa.
Jan-Emmanuel De Neve, ambaye ni mhariri wa ripoti hiyo, anaelezea sababu zinazochangia ustawi wa mtu. (VCS 13298) (Jan-Emmanuel De Neve, m, in English: Wana rasilimali za kutosha, pato la taifa liko sawa, na wanagawana rasilimali walizo nazo kwa usawa.
Pia wanasambaza kipato kupitia shirika la Ustawi ambalo linahakikisha kila mtu ana kipato cha kutosheleza na hii inachangia kuwa na amani kisaikolojia, na inachangia jinsi mtu anavyohisi.
Pia wanaishi maisha mema, mfumo wao wa kutoa huduma za afya ni bure kwa kila mtu, na la muhimu wanasaidiana wenyewe.
Wanaaminiana kama jamii na mashirika tofauti.
Ripoti imeweka bayana kuwa furaha imekuwa ikipungua miongoni mwa mataifa ya Ulaya na Marekani, hii ikichangiwa na kutoaminiana na joto la kisiasa katika mataifa hayo.
lakini katika taarifa njema ni kwamba kote duniani watu wameanza kuwa wakarimu ikilinganishwa na awali.
Linapokuja suala la kuwa na furaha, mataifa ya Nordic yamekuwa yakiongoza kwa kuwa na furaha zaidi.
Marekani imeshuka na kuchukua nafasi ya ishirini na nne katika mataifa yenye furaha zaidi duniani.
Mataifa matano ambayo hayana furaha kote duniani ni Afghanistan, Sierra leone, Lebanon, Malawi, na Zimbabwe.