
Flaqo ambaye alijulikana sana kwenye tasnia ya ugizaji kwa kutumia majina ya Baba Otis na mama Otis ameeleza kwamba kama kazi yoyote ile hakuna mafanikio yasioandamana na changamoto.
Muigizaji Flaqo na Trisha Khalid pia walijadili wazi kuhusu uhusiano wao wakati wakiwa kwenye mahojiano na wanahabari. Wanahari hao walitaka kujua iwapo wawili hao wako kwenye mahusiano.
"Wakiendelea ivo wanabanti, Flaqo ni mtu mzuri," alisema Trisha Khalid.
Flaqo kwa upande wake amemtaja Trisha kama mtu mzuri sana na ambaye amemsaidia pakubwa kupata nafasi katika tasnia ya maigizo na mambo mengine kadhaa.
"Napenda kufanya kazi na Trisha maana ana talanta ya kipekee na pia ni mrembo. Amenipea nafasi nyingi sana za kazi na mimi pia nimefanya hivyo kwake na ni furaha," alizungumza Flaqo.
Hata hivyo muigizaji huyo ameonesha furaha na hatua ambayo amepiga kwenya maigizo akieleza kwamba kwa sasa comedi zake zinaoneshwa kwenye runinga ya NTV.
"Inafurahisha sana kujiona hapo kwa runinga, Tulianzia huko nyuma kabisa na kujiona hapa namshukuru mwenyezi Mungu. Nashukuru wale wafwasi wangu ambao wanaendelea kuniunga mkono. Naendela kujituma nina furaha sana, ahasanteni sana,' aliweka wazi.
Flako pia amewapa shukrani waigizaji wachanga wanaoendela ana kuwataka kuendela kujituma na wasiwe watu wa kukata tamaa.
"Kile naaeza ambia waigizaji wachanga ni kwamba, jitume, jisimame hakuna mtu atakuja kukusaidia. Kuna wakati ata mimi nilikuwa nakwama sana nakosa mwelekeo. Changamoto lakini nilikuwa nakaa kimiya na sikutaka kuyazungumzia," alieleza.