Rubia ambaye ameeleza kwamba anatoka katika kaunti ndogo ya Lugari amefichua masaibu makubwa aliyokumbana nayo katika maisha yake ya ujana jambo ambalo lilimfikisha kwa maamuzi yasiyo ya busara.
Ameeanza na kuweka wazi alivyodanganywa kwamba atapewa kazi nzuri ya fedha za kutosha, jambo ambo lilimfanya kuawazia kubadilisha maisha yake kabisa na kutoka kwa umasikini ambao uliuwa unamwandama.
"Nilikutana na vijana nikiwa Mombsa, wakaniambia kuna mahali wanataka vijana. Nikapelekwa mahali panaitwa Sabasaba, wasichana wanajiuza na wavulana wanajiuza. Mimi nilipofika nikajua nimepona na sasa nitakuwa na pesa. Wanipelea kwa akina mama wawili wakanitambulisha," aleleza Rubia.
Baada ya kufanyishwa mazoezi ya gym na kula vizuri kwa wiki mbili kisha tukapelekwa kuanza kutizama video za uchi. Tukaanza kuoneshwa jinsi ya kuigiza michezo hiyo kwa siku saba mfululizo, mchana na usiku unalala kama masaa tatu na kuna vyakula unapewa kula.," aliongeza.
Mchungaji huyo pia amewataka watu kuwa maakini sana wanapoahidiwa msaada kutoka kwa watu kwani wengine lengo lao ni kukuletea matatizo zaidi ya yale ulionayo. Ameweka wazi kwamba maisha yake tangu mwanzo amepitia masaibu makubwa mengine kutoka kwa watu wa karibu wa uko wake.
"Tulkuwa tunapelekwa kwa pub, wasicha wanacheza bila mavazi, na mimi nikaona hii kazi ni nzuri sana ni kama Mungu amenisaidia. Ilifika wakati wa kwenda ofisini sasa wakasema waanze na mimi," aliendelea zaidi
"Akakuja mama mmoja ambaye namjua vizuri sana, tena mama wa mchungaji wa kanisa kubwa sana Nairobi. Nikambiwa huyo mama mwende mongee na yeye lakini sikujuwa wanaongea nini, Lakini mmedungwa madawa ukiguzwa tu itabidi mfanye vile anataka, na hiyo ndiyo ilikuwa kazi yangu ya kwanza," aliweka wazi mchungaji huyo.
Licha ya kazi hiyo kumfurahisha mwanzoni amefichua kwamba ilikuwa na masharti magumu sana. Na kuyakiuka ilikuwa kukosea hata zaidi, na ilimbidi ajifunze kuwa maakini sana.
"Kila dakika zilikuwa na peza zake. Walikuwa wanakuja watu wa kila aina, wazungu kwa wafrika, wakristu kwa waislamu. Nilikuwa naenda na watu watatu au wanne kila siku na sioni kuchoka sababu ya madawa. kila mzunguko ilikuwa ni 3k. Kulikuwa na CCTV na kengele, kwa hivyo huwezi pitisha muda ambao wamekubalina na mdosi wako. mchungaji huyo alieleza zaidi.