logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Aimbe ya Kihindi" Karen Nyamu ajibu baada ya Samidoh kudaiwa kumuimbia 'Bado nakupenda'

Katika wimbo huo, Samidoh anaimba kuhusu mwanadada  aliyemwavunja moyo.

image
na Samuel Maina

Burudani09 February 2023 - 05:28

Muhtasari


  • •Katika wimbo huo, Samidoh na Prince Indah wanaimba kuhusu mwanadada ambaye aliwavunja moyo na kumhakikishia kuwa mapenzi bado yapo.
  • •Seneta huyo wa kuteuliwa alijibu, "Aimbe ingine sasa ya kihindi nifikirie hio mambo," 

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh ameachia wimbo mpya wa mapenzi na mwenzake wa Ohangla Prince Indah.

Wimbo 'Bado Nakupenda' ambao umefanywa vizuri kwa mtindo wa mchanganyiko wa Mugithi na Ohangla ulichapishwa  kwenye mtandao wa YouTube siku ya Jumatano na mashabiki wengi wameweza kuupokea vyema.

Katika wimbo huo, Samidoh na Prince Indah wanaimba kuhusu mwanadada ambaye aliwavunja moyo na kumhakikishia kuwa mapenzi bado yapo.

"Hata kama ulienda mbali nami, bado nakupenda. Hata kama uienda mbali nami, bado nakuenzi," korasi ya wimbo huo inasema. 

Mamia ya wanamtandao wameendelea kutoa hisia mseto kuhusu wimbo huo uliofanywa kwa lugha ya Kikuyu, Kijaluo na Kiswahili.

Baadhi wameibua madai kwamba Samidoh alimwimbia mzazi mwenzake Karen Nyamu katika wimbo huo mpya.

"Naskia muibi wa nyimbo amekuibia wibo c ushike simu muongee kidogo kamamii ama unataka wimbo upotelee tu hifio🤔," Wakiende Hannah alitoa maoni chini ya chapisho la Karen kwenye mtandao wa Facebook.

Seneta huyo wa kuteuliwa alijibu, "Aimbe ingine sasa ya kihindi nifikirie hio mambo,"

Mkewe Samidoh, Edday Nderitu pia alihusika sana katika kuutangaza wimbo huo mpya kwenye mitandao ya kijamii.

Huku akiwaomba wafuasi wake kuutazama wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube, Bi Nderitu alimhakikishia mume wake kuwa mapenzi yake kwake bado yapo.

"Umesema ulikua mtoto, na je mimi? We simu utapiga piga.. mi bado nakupenda Samidoh," alisema kwenye Facebook.

Karen alitangaza mwisho wa uhusiano wake na Samidoh katikati mwa Desemba kufuatia tukio la ugomvi uliomhusisha yeye, baba huyo wa watoto wake wawili na mke wake Edday Nderitu  katika eneo moja la burudani jijini Dubai.

"Wanawake wakubwa na wajasiri watathibitisha kwamba mara nyingi kiungo chetu dhaifu ni wanaume tunaojihusisha nao. Ninaacha mtindo huo," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram mwezi jana.

Aliongeza "Nimefanya uamuzi wa kusitisha uhusiano wangu na baba wa watoto wangu na sasa ni mpenzi wa zamani."

Nyamu alibainisha kuwa hakuwa na majuto yoyote kufuatia  kile kilichotokea Dubai, na kuahidi kuwa tukio hilo lilikuwa la mwisho.

"Sitamani ningefanya mambo kwa njia tofauti," Nyamu alisema. "Najua nilipaswa kumpigia simu na kumaliza kimya kimya, lakini niliamua kuweka hadharani kama jinsi tu drama mambo tatanishi yamekuwa," aliongeza.

Hapo awali, Karen Nyamu, Samidoh na Edday Nderitu walikuwa wamehusika katika ugomvi ambao ulirekodiwa na video kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Wakenya watumizi wa mitandao ya kijamii walizungumza kuhusu drama hiyo kwa siku kadhaa huku wakitoa maoni tofauti kuhusu yaliyotokea.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved