"Alikuwa anadungwa sindano 48!" Nonini azungumzia kifo cha kakake aliyefariki juu ya meza

Rapa huyo alisema kuwa marehemu alikata roho baada ya kukumbwa na shida ya mapafu.

Muhtasari

•Nonini alifichua kuwa Jude aliugua TB kwa muda mrefu kiasi kwamba ugonjwa huo ulisambaa sehemu nyingine za mwili na kuwa hatari zaidi.

•Alifichua kuwa ugonjwa wa kakake ulikuwa mbaya sana hivi kwamba madaktari walilazimika kumwekea dawa mwilini kutumia sindano nyingi.

NONINI
Image: HISANI

Mwanamuziki maarufu wa Kenya Hubert Mbuku Nakitare almaarufu Nonini amefunguka kuhusu kifo cha kaka yake mzaliwa wa kwanza aliyefariki miaka mingi iliyopita.

Wakati akishiriki mazungumzo na Mwafreeka kwenye podikasti ya Iko Nini, rapper huyo ambaye kwa sasa anaishi Marekani alifichua kuwa kaka yake Jude Nakitare alifariki kutokana na ugonjwa wa TB.

Nonini alifichua kuwa marehemu Jude aliugua TB kwa muda mrefu kiasi kwamba ugonjwa huo ulisambaa sehemu nyingine za mwili na kuwa hatari zaidi.

“Ndugu yangu alikuwa na TB. TB zamani ilikuwa ni noma. Ilikuwa imejirudia,” Nonini alisema.

Msanii huyo alifichua kuwa ugonjwa wa kaka yake ulikuwa mbaya sana hivi kwamba madaktari walilazimika kumwekea dawa mwilini kwa kutumia sindano nyingi ili kuokoa maisha yake.

“Unajua TB ikikushika utibiwe, alafu ikushike tena utibiwe, huwa inaanza kususia dawa. Inabidi umeanza dawa kutumia sindano. Mazee alikuwa anadungwa sindano nyingi, alikuwa anadungwa nadhani sindano 48. Lakini ikirudi tena sindano lazima ziongezewe,” alisema.

Nonini alisema kuwa marehemu alikata roho baada ya kukumbwa na shida ya mapafu.

“Siku moja alikuwa na shida ya mapafu. Alishindwa kupumua. Alikufa juu ya meza walipokuwa wakijaribu kumfufua. TB ilikuwa noma. Ukiskia TB ina tiba, zamani ilikuwa ngori,” alisema.

Rapa huyo alifichua kwamba alikuwa bado shuleni wakati kaka yake alipofariki. Marehemu alikuwa tayari mtu mzima na alikuwa akifanya kazi wakati alipoteza maisha yake.

Takriban muongo mmoja uliopita, Nonini alitoa wimbo ‘Waliotuacha’ ambapo alizungumzia kifo cha kakake na kuzungumzia jinsi mamake alivyokuwa akimlinganisha na marehemu.

Tazama baadhi ya maneno ya wimbo huo;

Naskia kulia nikiskia sauti ya hiyo guitar,

Pia nakumbuka mathangu saa zingine vile huniita,

Jina ya marehemu brother yangu jo, mkubwa,

Alituacha kabla hata mimi jo sijakua mkubwa,

Kabla hata hii local watu hawajaanza hata kuskia,

Local? Ah (nkt!)

Kabla ata hii genge haijakubaliwa kabisa,

Ndio maana siku hizi ata siendangi kanisa,

Ile uchungu mi huskia nikimwona kwa picha,

Ile uoga mi huskia nikitembea bila yeye kwa giza,

Jamaa mkiona saa zingine sitaki kucheka,

Msichukulie eti Nonini siku hizi anatulenga,

Ni vile tu nikicheka jo hiyo mcheko yangu,

Hutoka exactly tu ka ile ya brother yangu, eeh,

Jamaa moja alikuwa mtu wa reggae damu,

Na-wish pia angekuwa hapa askize ngoma zangu,

Ingembamba kila siku kufungua gazeti anione hapo,

Akiwasha TV aone ngoma ananikuta ndani bado,

Ye ndio hunipa roho ya kuandika ngoma mambo bado,

Na hii verse wacha tu niimalize hapo.