Alinur aahidi kumsaidia Mboya baada ya kutemwa na mpenziwe

Baada ya kufahamu kuachwa kwake na mpenzi wake,mwanasiasa huyo ameapa kumsaidia

Muhtasari
  • "Nilitabiri mambo hayatamwendea vizuri  Kevin Mboya na baada ya kutazama video yake kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii
ALINUR MOHAMED
Image: KWA HISANI

Mwanasiasa maarufu wa Kenya anayejulikana kama Alinur Mohammed ameahidi kumpeleka mwanamitandao anayevuma, Kevin Mboya hadi Dubai kwa likizo na kumpa posho ya Ksh 700,000 kwa matumizi yake.

Kulingana na mwanasiasa huyo, alitabiri kuwa mambo hayangemwendea vyema Kevin Mboya alipofunga safari ya kuenda Kwale kumuona mpenziwe kisha kutoweka kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kufahamu kuachwa kwa Mboya na mpenzi wake, mwanasiasa huyo ameapa kumsaidia kupona jeraha la moyo kwa kumlipia likizo ya wiki moja Dubai na kumpa Ksh 700k kwa matumizi yake.

"Nilitabiri mambo hayatamwendea vizuri  Kevin Mboya na baada ya kutazama video yake kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii, nimethibitisha hofu yangu. Lakini yaliyopita si ndwele. namtafuta. Nitamlipia likizo yake ya wiki moja huko Dubai na kumpa KSH. 700k kwa matumizi yake,"Alinur aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mboya alivuma sana mitandaoni wikendi iliyopita, baada ya kusafiri hadi Kwale kwa mpenzi wake, lakini baada ya kufika kipusa huyo hakuweza kupokea simu zake wala kujibu jumbe zake.