Siku ya Alhamisi, mwimbaji mzaliwa wa Pwani Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo alijibu haraka baada ya aliyekuwa mpenzi wake, mwanasosholaiti Vera Sidika kukataa kutumbuiza kwenye jukwaa moja naye wikendi ijayo.
Muda mfupi tu baada ya mlimbwende huyo maarufu kutangaza kwamba hatahudhuria tamasha ambalo wote wawili walikuwa wamealikwa kama wageni maalum, Brown Mauzo aliwasasisha mashabiki wake akifichua kuwa mpenzi wake mpya, Kabinga Jr angeandamana naye badala yake.
“Kuna nini watu wangu wa Mwea.. Mimi na mpenzi wa maisha yangu tutaonekana kwenye Jamii Garden Jumamosi hii. Njooni mfurahie hafla mbaya zaidi wikendi hii,” Mauzo alisema chini ya bango jipya aliloshiriki kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Katika bango hilo jipya, picha ya Vera Sidika ilikuwa imefutwa na nafasi yake kuchukuliwa na picha ya anayedaiwa kuwa mpenzi mpya wa mwimbaji huyo, ambaye pia anasemekana kuwa rafiki mkubwa wa Otile Brown.
Mapema siku ya Alhamisi, Vera alikuwa ametoa tangazo maalum kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwafahamisha mashabiki wake kwamba hatahudhuria tamasha la Mwea kama ilivyotangazwa awali.
Katika tangazo lake, mama huyo wa watoto wawili alidai kwamba vyombo fulani vya habari na baadhi ya watu walikuwa wakiripoti vibaya kuhusu tamasha hilo ili kufaidika na hali ya sasa ya familia yake, akiweka wazi kwamba hatahudhuria.
"🚨VERA SIDIKA IMEFUTWA🚨 Imefahamika kuwa baadhi ya watu binafsi na blogu zinatangaza tamasha fulani yangu na Ex wangu mjini Mwea," Vera Sidika aliandika kwenye Instagram.
Aliongeza, “Ningependa kuwafahamisha mashabiki wangu na umma kwa ujumla kwamba aina hii ya utangazaji ni ya kupotosha na ni ya udanganyifu iliyoundwa katika muundo ili kufaidika na hali ya familia yangu ya kibinafsi. Tafadhali kumbuka kuwa sitahudhuria au kujitokeza.
Haya yanajiri zaidi ya miezi miwili baada ya habari za kutengena kwa wawili hao.
Mwishoni mwa mwezi Agosti, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.
"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.
"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.
Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.
“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"