Mafisi poleni!Kutana na mpenzi wake msanii Nadia Mukami

Muhtasari
  • Msanii Nadia Mukami ni mmoja wa wasanii ambao wametia bidii katika tasnia ya burudani licha ya kuwa na changamoto tofauti
  • Hongera sana Nadia, kamati ya mafisi poleni ashaanyakuliwa na mwingine
nadia-mukami-341
nadia-mukami-341

Msanii Nadia Mukami ni mmoja wa wasanii ambao wametia bidii katika tasnia ya burudani licha ya kuwa na changamoto tofauti.

Wengi wamekuwa wakiuliza msanii huyo kama anampenzi lakini leo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amewashangaza mashabiki wake baada ya kupakia picha ya mpenzi wake huku akimsifia.

Kulingana na msanii huyo Mpenzi wake ambaye alimtambulisha kama Priyan amekuwa naye kwa njia zake panda na katika changamoto zake.

"Licha ya kila kitu walichosema juu yangu leo, umenioga kwa upendo mimi natabasamu tu hapa karibu na wewe

Kuwa katika umaarufu, unahitaji mtu anayekupenda, Mtu anayekuona nje ya umaarufu, pesa, umakini, uvumi, mazungumzo na matusi

Mtu ambaye anazungumza na nafsi yako na wewe ni hivyo tu! Nilipaswa kukutana nawe mapema ili nipate aina hii ya mapenzi lakini najua haijachelewa

Tunatoka makabila 2 tofauti lakini Upendo wetu unashinda hilo! NAKUPENDA SANA PRIYAN💕,"Aliandika Nadia.

Hongera sana Nadia, kamati ya mafisi poleni ashaanyakuliwa na mwingine.