Michelle ni rafiki wangu wa karibu-Makena aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Mwandishi wa zamani wa BBC Makena Njeri amesema alikuwa akiishi uongo wakati alikuwa akichumbiana na wanaume
  • Makena alisema yuko sawa na watu wanaomwita "Chris au Christine"
Makena Njeri
Image: Studio

Mwandishi wa zamani wa BBC Makena Njeri amesema alikuwa akiishi uongo wakati alikuwa akichumbiana na wanaume.

Makena ambaye hivi karibuni alijitambulisha kama 'shoga' alimwambia Massawe Japanni kuwa yuko sawa na uhusiano wake wa sasa.

"Sitaki kuzungumza juu ya suala hili kwani hiyo ni historia yangu na pia ilikuwa uhusiano wa kibinafsi sana."

Aliongeza kuwa alikuwa chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa jamii.

"Shinikizo lilikuwa kubwa mno na nilikuwa naishi kwa uongo, na shida ni kwamba unaishia kumuumiza yule mtu mwingine."

Makena alisema yuko sawa na watu wanaomwita "Chris au Christine"

"Nina watu wanaoniita Chris na niko sawa na hilo."

Alipoulizwa juu ya kejeli kutoka kwa wanamitandao, Makena alisema;

"Niko sawa na maoni ya kila mtu. Inakuwa tu suala wakati inatumika kama silaha dhidi yako. ' Changamoto kubwa ni kwamba watu hawaelimishwi kuhusu jamii ya LQBTQ,"

Makena aliweka wazi kuwa Mitchelle sio mke wake, bali ni rafiki yake wa karibu.

"Ni makosa kubwa sana kumuita MItchelle mke wangu, uhusiano wangu na Mitchelle ni wa karibu sana, na sisi ni marafiki wa karibu

Ukiena kwenye mitandao yangu ya kijamii ya instagram nipakia picha za watu wengi,naishi maisha yangu kwa uwazi, kama kuna wakati utafika nimtambulishe mke wangu hadharani nitafanya hivyo." Alisema Makena.