'Simfeel kabisa,'Benpol asema hana hisia zozote za Anerlia Muigai

Muhtasari
  • Benpol asema hana hisia zozote za Anerlia Muigai
  • Ndoa kati ya msanii Ben Pol na Anerlisa Muigai ilikuwwa ya kupigiwa mfano na kutamanika na wengi mitandaoni
gVUk9kpTURBXy80NTA3YjEwNDQxOGFhMDQ1MTFlOGFiZDU2NDk5MDJiZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
gVUk9kpTURBXy80NTA3YjEwNDQxOGFhMDQ1MTFlOGFiZDU2NDk5MDJiZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Ndoa kati ya msanii Ben Pol na Anerlisa Muigai ilikuwwa ya kupigiwa mfano na kutamanika na wengi mitandaoni.

Wawili hao walivishana pete ya uchumba mwaka wa 2019, mwaka 2020 Aprili walifunga pingu za maisha, na kufanya harusi ya kifahari iliyo hudhuriwa na watu wachache.

Benpol akiwa kwenye mahojiano alikiri kwamba hana hisia zozote za kimapenzi kwa Anerlisa Muigai.

“Kwa saa hivi mimi namuombea tu heri lakini kusema ati namzimia, hapana hakuna kitu kinaweza kutokea kati yangu mimi na yeye

Simfeel kabisa, unfortunately, sidhani kama ni kosa, huo ndo ukweli wangu

Alinitumia kabisa makaratasi ya wana sheria kuhusu separation and I was scared…hapo vitu vilikuwa vimeharibika sana

Baadaye vitu vikarudi kutoka September mpaka October ndo tukawa tumerudi. Vitu vikaenda vizuri mpka mwezi wa pili mwaka huu February ndio vitu vikapasuka tena.

I did my best hata muda ukirudi nyuma, ningefanya vile vile, hamna kitu ambacho ningerekebisha, kwa hiyo kama vitu havijaenda ni mipango ya mungu tu na huwezi badilisha

Whatever happened in the two years, ilikuwa tu imepangwa na Mungu, maana kila mtu alikuwa alivyo na familia zilikuwa zinatusapoti," Alisema Ben pol.

Msanii huyo pia alisema kwamba wakati huo ulikuwa mgumu sana katika maisha yake.

“Kipindi hicho kilikuwa kigumu sana…mpaka majira ya siku yalibadilika, yaanni kuna wakati nilikuwa naamka saa kumi na moja join ndo nakunywa breakfast, na kula lunch saa tatu usiku, dinner saa tisa Usiku, nalala sa kumi na moja.

Lakini I did a lot of work to be Okay. ..I was invested kweli kwenye mapenzi and I gave my all, saying this I my wife so went thing went south I was hurt”.