'Siwezi subiri kuwaona malaika wangu,'Diamond asema baada ya kuwasili Afrika Kusini

Muhtasari
  • Diamond awasili Afrika Kusini kuwaona wanawe
  • Miezi chache iliyopita msanii huyo alienda kuwatembelea wanawe a kuwa na wakati mwema na wao
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwajulisha mashabiki wake kuwa amewasili Afrika Kusini vyema na kuwa hawezi ngoja kuwaona wanawe ambao aliwatambulisha kama malaika wake

Staa wa bongo Diamond Platnumz kwa mara nyingi ameenda Afrika Kusini kuwaona wanawe Princess Tiffah na Prince Nillan.

Miezi chache iliyopita msanii huyo alienda kuwatembelea wanawe a kuwa na wakati mwema na wao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwajulisha mashabiki wake kuwa amewasili Afrika Kusini vyema na kuwa hawezi ngoja kuwaona wanawe ambao aliwatambulisha kama malaika wake.

"Nimewasili Afrika Kusini vyema siwezi subiri kuwaona malaika wangu 🚀 @princess_tiffah @princenillan ❤️," Aliandika Diamond.

Wiki iliyopita mwanawe Diamond Princess Tiffah alilia ili apelekwe nchini Tnaznia ambapo, Mama Dangote alimsihi Zari ampelekee mjukuu wake.

Je kuna uwezekano mkubwa kwamba Diamond na Zari Hassan wanaweza rudiana na kuwa wazazi bora kwa watoto wao?

Kama tunavyojua ni kwamba Zari hana mpenzi na pia Diamond hana mpenzi wa roho yake, maoni yako ni yapi kama wawili hao wanaweza rudiana?