Mungu alijua ni wangu,'Vera Sidikia amshukuru Mungu kwa kumtenga Mauzo awe mumewe

Muhtasari
  • Vera Sidikia amshukuru Mungu kwa kumtuma Mauzo awe mumewe
VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
VERA SIDIKA NA MPENZIWE BROWN MAUZO
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti na mjasiriamali mashuhuri Veronica Mung'asia almaarufu kama Vera Sidika kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameweka wazi kwamba Mungu alimtuma Mauzo awe mume wake na alijua kwamba ni chaguo lake.

Pia kupita kwenye kipindi cha Q &A  instgrama mwanasosholaiti huyo alifichua kwamba msanii Mauz alimpoteza baba yake akiwa na umri mchanga.

Vera alisifia Mauzo kwa kuwa bora katika michezo ya kitandani.

Alisema kwamba anampenda mumewe sana, haya yanajiri baada ya miezi chache kupita baada ya Vera kufichua jinsia ya mwanawe.

Mapema wiki hii Vera aliwasuta wanamitandao ambao walisema kwamba uhusaino wake na Mauzo hautadumu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera amesema kuwa walichumbiana kisiri na mpenziwe kwa kipindi cha miezi miwili kabla ya kuweka uhusiano wao hadharani.

"Nampenda sana, kusema kweli moyo wangu, ubavu wangu,Mungu alijua kwamba ni wangu na ni yeye

Ndio maana aliokoa bora kwa kuwa wa mwisho," Aliandika Vera Sidika.

Siku ya Alhamisi, Agosti 12 Vera na kipenzi chake Brown Mauzo waliadhimisha mwaka mmoja wa ndoa yao.

Wawili hao walijitosa kwenye ndoa mnamo Agosti 12 mwaka uliopita na mapenzi yao yameendelea kunoga huku sasa wakiwa safarini kuanzisha familia ndogo.