Usiache 'slay queens' tu wapate joto ya baby daddy,'Ushauri wake Akothee kwa akina mama

Muhtasari
  • Msanii Akothee kwa mara nyingine amewapa ushauri akina mama ambao wametengana na waume zaio ilhali wana watoto pamoja
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii Akothee kwa mara nyingine amewapa ushauri akina mama ambao wametengana na waume zaio ilhali wana watoto pamoja.

Kulingana na msanii huyo, akina mama wanapaswa kuwaruhusu watoto wao wawaone baba zao, na wala sio kuachia Slayqueens kitambi cha baba wa watoto wao wacheze nacho.

Aliandika haya baada ya kupakia video ya manawe akicheza na baba yake;

"Nitamwamia Oyoo nini leo akiniuliza kwa nini hawezi muona baba yake ilhali yuko hai,akina mama kuna pengo ambalo huwezi jaza maishani mwa mtoto wako

Usiachie slayqueens tuu wapaye joto ya baby daddy ,wacha watoto wa enjoy baba Yao kama angalia hai 🤣🤣🤣💃🧖💃💃💃

Mimi so mtoto wako ,huwezi no piga ,oba vile oyoo ana pasa kitambi ya babake 🤣🤣," Akothee alinakili.

Haya yanajiri huku Akothee akifichua kwamba wanawe wanasafari hii leo, huku akisema kwamba anaskia uchungu sana.

"Huwa tunapunguza maumivu kwa njia tofauti,watoto wangu wanasafiri leo na siwezi eleza uchungu na maumivu ambayo naskia

Nitawaambia siku moja kwa nini ni hivyo."