'Mapacha wanakuja,'Arrowbwoy amjibu Nadia Mukami baada ya kumwambia anataka watoto

Muhtasari
  • Arrowbwoy amjibu Nadia Mukami baada ya kumwambia anataka watoto
Image: INSTAGRAM//NADIA MUKAMI

Msanii Nadia Mukami ambaye alizindua ubabe wake katika fani ya muziki kwa ngoma yake ya 'radiolove' alimwandikia mpenziwe ujumbe akimwambia anataka watoto naye.

Uvumi umeenea sana kwamba wawili hao ni wapenzi, jambo ambalo Nadia alithibitisha na kusema wamekuwa pamoja kwa muda.

Kulingana na Nadia mpenzi wake anawachelesha wanawe kuenda shule,huku akikiri kwamba anampenda sana arrowbowy.

Ni ujumbe ambao uliwaacha wanamitandao midomo wazi.

"Thamani kuu watoto wetu watakopa kutoka kwetu ni Roho wa Kufanya Kazi kwa bidii! Ninasema kila wakati, sio juu ya kuwa bora zaidi juu ya kuitaka ZAIDI!

Kuna nyakati ambazo hatuwezi hata kuonana kwa muda mrefu na tuko katika Nairobi hii, Nairobi๐Ÿ˜Bana, unachelewesha watoto kuanza shule๐Ÿ™ˆ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜ Nakupenda sana @arrowbwoy," Nadia aliandika.

Baada ya msanii Arrowbwoy kuona ujumbe wake Nadia alimjibu na kumwambia kwamba mapacha wanakuja, kwa hivyo asitie shaka.

"Basi Leo tukosane lakini kesho Tusiachane my Queen @nadia_mukami Nakupenda zaidi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ Tulia Twins loading ๐Ÿ˜ƒ."

Kwenye mitandao yake ya kijamii, Nadia alisema kwamba aliamua kutangaza uhusiano wake mitandaoni kwa sababu anajihisi kwamba ni mtu amekomaa.

Haya basi kwa wale walikuwa wanadhani ni kiki ni wazi kuwa kwamba wawili hao ni wapenzi.