logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Nimepokea picha za sehemu za mwili kutoka kwa wasichana,'Alfred Mutua aweka mambo haya wazi

Wawili hao kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii walitangaza kutengana kwao.

image
na Radio Jambo

Habari25 August 2021 - 12:44

Muhtasari


  • Gavana wa Machakos Dr Alfred Mutua alivuma sana mitandaoni wiki jana baada ya kuachana na mkewe Lilian Ng'ang'a

Gavana wa Machakos Dr Alfred Mutua alivuma sana mitandaoni wiki jana baada ya kuachana na mkewe Lilian Ng'ang'a.

Wawili hao kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii walitangaza kutengana kwao.

Hata hivyo, siku chache baadaye walionekana katika sherehe ya  siku ya kuzaliwa ya Mutua 51 ambayo alifanya pamoja na mwimbaji Rayvanny.

Walionekana wakiwa na furah, huku baadhi ya wanamitandao wakisema kwamba hawajaachana.

Huku akizungumzia kuachana kwao akiwa kwenye mahojiano na Bonga na jalas, alikuwa na haya ya kusema;

"Tulikubaliana na Lilian si kushughulikia masuala yetu kwa umma. Yote ninayotaka kusema ni hii, mara moja umempa maisha yako kwa mtu kwa muda mrefu, inakuwezesha kuzingatia mambo mazuri ya wakati wako pamoja badala ya matatizo yoyote madogo ambayo unaweza kuwa nayo

Ni muhimu sana katika mahusiano mnaheshimiana wakati mnapokuwa pamoja au wakati hamyuko pamoja na kuacha nafasi ya upatanisho na urafiki ili hata kama wewe na washirika wengine bado unaweza kubaki marafiki na kufanya kazi pamoja," alisema Mutua.

Gavana Mutua pia alisema kuwa simu yake haijapumzika baada ya kutangaza kuachana kwake na Lilian.

Kiongozi huyo alisema kuwa alikuwa akipokea jumbe nyingii kwenye simu yake, baadhi yao kuwa sehemu za mwili.

Pia laiwashukuru wote ambao wamekuwa wakimtumia jumbe za kumtia moyo.

"Nataka kuwashukuru wale ambao wameandika kwangu, nimepata DMS nyingi ambazo baadhi ni za ajabu sana na wengine wametuma sehemu za mwili."

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved