Marya Prude azungumzia jinsi wazazi wake walimlinda baada ya ndoa yake kuvunjika

Muhtasari
  • Marya Prude azungumzia jinsi wazazi wake walimlinda baada ya ndoa yake kuvunjika
prude-Marya7-696x522
prude-Marya7-696x522

Hakuna mzazi ambaye hutamani kuona mwanawe akiwa katika wakati mgumu, au kuona mwanawe akipena talaka na mumewe au mkewe.

Mary Irungu maaraufu Marya Prude, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha yake baada ya kupeana talaka na Willis Raburu.

Marya akiwa kwenye mahojiano na mpasho, alisema kwamba wazazi wake walimchunga na walihakikisha yuko sawa baada ya talaka.

Marya alikuwa akipitia mchakato wa talaka na alikuwa akipona kutokana na kumpoteza binti yake, Adana.

"Kufikia wakati huo nilichohitaji tu ni tiba na kujali afya yangu ya kiakili tu. Alinitunza na mama yangu alihakikisha ninakula na kulala. Yeye angenipikia kila kitu na kuniambia nikae nao," Alisema.

Marya alisema kuwa familia yake ina uhusiano wa karibu na kama mzaliwa wa kwanza, mara nyingi, wazazi wake na ndugu zake hutafuta ushauri wake wanapotaka kufanya maamuzi anuwai.

Alielezea pia kuwa wazazi wake pia sio wakali sana kuwazuia watoto wao kufurahiya maishani.

"Kama kwa mfano, baba yangu alininunulia kinywaji cha kwanza cha kileo. Alinijulisha kwa hiyo. Alikuwa kama," Unapokuwa nje na marafiki wako, chukua hii na epuka kinywaji hiki au vinginevyo la sivyo utaishia kuumwa na kichwa. Nakadhalika."

Akizungumzia jinsi alivyokuwa wazi kwa wazazi wake juu ya uhusiano, Marya alisema baba yake hajawahi waona wapenzi wake.

Pia alisema kwamba alikuwa anazungumza mambo ya uhusiano wa kimapenzi na mama yake.