Kile watu hawajui ni kwamba nilikuwa nimepoteza ujauzito mwingine mnamo 2018- Marya Prude afunguka

Muhtasari
  • Sio kila mama ambaye amebarikiwa kukutana na watoto wao hata baada ya kujitahidi katika safari yao
  • Marya Prude, kwa mara ya kwanza amefunguka, na kufichua kwamba hakupoteza mtoto mmoja bali wawili
Marya Prude
Image: Maktaba

Ni furaha na matamanio ya kila mama mwenye ujauzito, kuona mwanawe au kiumbe ambacho amekuwa akibeba kwa miezi 9.

Sio kila mama ambaye amebarikiwa kukutana na watoto wao hata baada ya kujitahidi katika safari yao.

Kuna wanawake mimba zao hutoka mapema, na hata wengine kujifungua watoto wao wakiwa wamekata roho.

Marya Prude, kwa mara ya kwanza amefunguka, na kufichua kwamba hakupoteza mtoto mmoja bali wawili.

Aiwa kwenye mahojiano na mpasho Prude alisema kwamba mimba yake ya kwanza ilitoka mapema.

Katika kipindi hicho hicho, ndoa yake na  Willis Raburu ilimalizika.

"Mtoto wangu alikufa tumboni baada ya shida kadhaa,Ilikuwa mimba ya wiki 9 na kwa hivyo, nilikuwa katika uchungu kwa zaidi ya masaa 12-14, nilijifungua kawaida. Nilisukuma mara tatu na mtoto akatoka nje akiwa amekufa." Alifunguka.

Marya aliendelea kusimulia kwamba wawili hao walitarajia wangeweza kukutana na mtoto wao baada ya kupoteza mtoto wa kwanza kupitia kuharibika kwa mimba yake ya kwanza.

Alisema ilikuwa ni ujauzito wa kiinitete. [Aina ya ujauzito wa mapema ulioshindwa, ambapo kifuko cha ujauzito hukua, lakini kiinitete haifanyi]

"Kile watu hawajui ni kwamba nilikuwa nimepoteza ujauzito mwingine mnamo 2018 kwa wiki tisa kisha, mnamo 2019, nilipata ujauzito na mtoto Adana," alisema.

Ilikuwa ngumu sana kwetu kwani tulikuwa tukijaribu kupata mtoto. "

Akizungumzia safari ya ujauzito, Marya alisema alikuwa na ujauzito mzuri na dada yake hata alimfanyia sherehe ya kuonyesha jinsia.

Marya hapo awali alikuwa akijulikana kuwa Mkristo mwenye nguvu na mwamini, lakini baada ya kupata hasara, imani yake ilisita.