Hongera!Muigizaji Daddie Marto abarikiwa na mtoto wa pili

Muhtasari
  • Muigizaji Daddie Marto abarikiwa na mtoto wa pili
  • KUpitia kwenye ukuras wake wa instagram muigizaji huyo ambaye alifahamika sana kupitia kwa kipindi cha   Sue Na Johnnie  alitaja kwamba mkewe alijifungua mnamo Agosti 25, 2021 saa 02.15 asubuhi
Image: Instagram/Daddie Marto

Muigizaji mashuhuri Martin Githinji aka Daddie Marto na Mkewe Christine Koku Lwanga wamemkaribisha mtoto namba mbili katika familia yao.

KUpitia kwenye ukuras wake wa instagram muigizaji huyo ambaye alifahamika sana kupitia kwa kipindi cha   Sue Na Johnnie  alitaja kwamba mkewe alijifungua mnamo Agosti 25, 2021 saa 02.15 asubuhi.

Mtoto wao alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.385,kulingana na muigizaji huyo.

Katika ujumbe wake Daddie Marto alisema kuwa walichukua muda mbali kwenye mitandao ya kijamii kurekebisha na kuzingatia kumtunza vizuri mtoto wao mchanga.

"Mabibi na Mabwana, wenye uzani wa 3.385kgs, saa 02.15 asubuhi mnamo Agosti 25, 2021 kifungu chetu cha furaha kilitua 😊 Tulichukua wakati wa kujirekebisha na kumjua, mtoto yuko sawa kwa kukula na kulala, baba amechoka lakini ananing'inia hapo ndani, mama anachukua kibao kikubwa lakini ilitarajiwa, kwa hivyo yote ni sawa. Tumebarikiwa kweli 😊 ”alishiriki Daddie Marto.

Habari ya Daddie Marto na mkewe kukaribisha mtoto wao wa pili ilipokelewa vizuri na sehemu ya mashabiki na wafuasi wao.

Wengi waliwatymia jumbe za pongezi.

Hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki;

blessednjugush: Congratulations!!!!!! Konge na meerî

hassansarah: Congratulations 👏🏽👏🏽👏🏽

kate_actress: Ariririiiiiiiiiii🙌🙌🙌🙏

millywajesus: Congratulations ❤️❤️

mojishortbabaa: Congratulations bro

foi_wambui_: Congratulations 🎊