logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilimpata mchana peupe,akimpa jamaa aliyemtambulisha kama binamu yake asali yangu-Mwanamume asimulia

Sijui ni seme kuna wale wamepewa damu ya kudanganya katika uhusiano wao,

image
na Radio Jambo

Habari02 September 2021 - 11:04

Muhtasari


  • Kuna sababu nyingi kwa nini wapenzi huachana, kuna baadhi ya wale huona uhusiano wao hauendi popote na kuamua kila mmoja aende njia zake
sad man

Kuna sababu nyingi kwa nini wapenzi huachana, kuna baadhi ya wale huona uhusiano wao hauendi popote na kuamua kila mmoja aende njia zake.

Sijui ni seme kuna wale wamepewa damu ya kudanganya katika uhusiano wao,licha ya kuwa na mpenzi au ni mazoea.

Nikiwa katika ziara zangu nilipatana na mwanamume mmoja na kunieleza kwa nii hana mpenzi na hatamani kuwa naye.

KUlingana na Thomas,30,alikata tamaa ya mapenzi baada ya kumpata aliyekuwa mpenzi wake na mwanamume kitandani miaka 5 iliyopita.

Thomas akisimulia hadithi yake alisema kwamba mpenzi wake alimtambulisha mwanamume huyo kama binamu yake.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa na mpenzi ambaye nilikuwa nampenda sana, alikuwa mpenzi wangu wa kwanza,tulichumbiana kwa miaka 3

Tabia zake zilianza kubadilika, siku moja nilimuuliza amekuwa akipakia picha za mwanamume sana mitandaoni akaniambia kwamba uyo ni binamu yake

Si kuwa na wasiwasi kwani nilikuwa na muamini sana kwani tulikuwa tumepanga mambo mengi naye

Siku ambayo nilimpata na mwanamume huyo, sitawahi sahau,nilimpata na mwanamume huyo mchana peupe kitandani wakifanya ngono

Mwanamume huyo hakuwa binamu wake bali alikuwa mpenzi wake, nilishindwa nami nilikuwa nani kwake

Si kutaka maelezo zaidi nilitoka na nikaenda, na hapo ndipo tuliachana na kukata tamaa ya mapenzi."

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved