'Wacheni afurahie matunda ya bidii yake,'Willy Paul ampongeza Juliani

Muhtasari
  • Ndoa ni ahadi ya maisha kati ya mume na mke na daima imewekwa na Mungu na pia ni mwanzo wa familia
  • Tunapozungumzia wanamuziki maarufu hatuwezi kukosa kumtaja Julius Owino maarufu kwa jina la Juliani
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Ndoa ni ahadi ya maisha kati ya mume na mke na daima imewekwa na Mungu na pia ni mwanzo wa familia.

Tunapozungumzia wanamuziki maarufu hatuwezi kukosa kumtaja Julius Owino maarufu kwa jina la Juliani.

Walakini, Juliani alikuwa gumzo baada ya uhusiano na Gavana wa Mke wa zamani wa Machakos Alfred Mutua Lilian Nga'ng'a.

Mwimbaji Willy Paul alimshauri Juliani kupitia kwa video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa instagram na akaendelea kusema kuwa watu wanapaswa kuacha Juliani afurahie matunda ya bidii yake.

Bali na hayo pia alimsifia Lilian kwa urembo wake.

"Watu mnapaswa kuachana na JUliani afurahie matunda ya idii yake,Juliani shikilia hapo buda,mtoto ni mzuri shikilia,"Willy Paul alisema.

Wawili hao siku ya Ijumaa walithibitisha, kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwamba ni wapenzi.

Unafikiria nini? Je! Juliani aliiba mke wa mtu au Lilian alimkubali? Tunapaswa kufanya nini kulinda ndoa zetu zisianguke?