Natamani tena kumpenda mtu-Diamond akiri huku akizungumzia kibao chake kipya

Muhtasari
  • Simba akiri anatamani kumpenda mtoto wa mtu
Diamond-e1531046176849-696x455
Diamond-e1531046176849-696x455

Staa wa bongo kwa mara nyingine siu ya Jumapili alivunja rekodi kwenye youtube baada ya kibao chake kupokea watazamaji zaidi ya elfu 100 kwa muda wwa dakika 45.

Baba wa nne inaonekana kuwa katika hali tofauti ya akili baada ya video yake ya hivi karibuni kwa jina la "Nitaanzaje".

Kupitia kwe ye ukurasa wake wa instagram msanii huo alikiri kwamba kibao hicho kinamfanya atamani kumpenda mtu tena.

Diamond anafahamika kama mwanamume ambaye hakai na mwanamke mmoja, kwani amekuwa kwenye uhusiano na wanawake tofauti.

KUlingana na Diamod aliutoa wimbo huo kwa maana alihisi mashabiki wake wamempeza kuimba kibao cha mapenzi.

Huu hapa ujumbe wake

" Nikiitazama hii video, hususan kipande hiki nakumbuka mbali sana...enzi za Mahaba mazito na Madam....Enzi ambazo tulikuwa tunajifungia chumbani wiki nzima, nakwepa kurecord na ata show ikitokea naitaftia sababu ya kutokuwepo....

kiukweli wimbo huu wakati nautoa, sikuuchukulia serious....niliutoa tu kama bonus kwakujua mashabiki zangu wamenimiss kunisikia nikiimba hivyo..

Licha ya kupokelewa na Kupendwa sana ulivyotoka...for some reason kadri muda uendanvyo nimejikuta naupenda saana, na mbaya zaidi kila niusikiapo unanifanya nitamani tena kumpenda mtu, na kuwa tena wenye Mahusiano......

japo ghafla akili timamu hunijiaga, na kunambia "Simba Jifocusie zako kwenye kazi mwaya "πŸšΆβ€β™‚οΈ .... #Naanzaje," Aliandika Diamond.

Ala je Diamond ana wazo la kumtafuta mpenzi wake wa maisha, na je akimpata uhusiano wao utadumu?