Mume wangu muhubiri alinifukuza baada ya kukataa aniletee mke mwenza-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mwanamke aeleza alivyofukuzwa na mumewe baada ya kukataa mke mwenza
sad woman
sad woman

Huwezi hukumu mwanamke baada ya kutoka katika ndoa yake kwani hujui nini haswa anapitia au amekuwa akipitia katika maisha yake ya ndoa.

Wengi husema kwamba ndoa za wahubiri ndio kamilifu, na kusahau pia wahubiri ni wanadamu na pia hufanya makosa.

Nikiwa katika ziara zangu, nilipata na mama peterson ambaye alinisimulia kwanini alitoka katika ndoa yake licha yake kuwa mkewe mhubiri.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilikuwa kwenye ndoa ambayo engi walidhani kwamba nilikuwa na furaha,lakini kile wengi hawakuelewa ni kwamba nilikuwa na uamuzi wangu

Mume wangu ambaye alikuwa muhubiri, kijijini baada ya kubarikiwa na watoto 2 naye alidai kwamba anataka ke mwenza na tayari ameshampata

Kile kilukuwa kimesalia ni mimi kumkubali, lakini nilikataa kwani singependa kumuona mume wangu na mwanamke mwingine

Na angekuwa mfano mwema kwa kanisa, lakini baada ya kukataa kwa muda mke mwenza alinifukuza usiku nikiwa na watoto wangu

Hapo ndipo nilikata tamaa ya ndoa na nikaamua kuwalea watoto wangu peke yangu."

KUlingana na mama huyo, hakujua kosa lake ili aweze kuletewa mke mwenza.