(+PICHA)Muigizaji Omosh ajiunga na chama cha UDA

Muhtasari
  • Muigizaji wa zamani wa kipindi cha Tahidi High Joseph KInuthia maarufu Omosh, amejiunga na chama cha kisiasa cha UDA
  • Omosh alivuma sana mitandaoni miezi chache iliyopita baada ya kuomba msaada kutoka kwa wakenya
Muigizaji Omosh na katibu mkuu wa chama cha UDA Veronica Maina
Image: Hisani

Muigizaji wa zamani wa kipindi cha Tahidi High Joseph KInuthia maarufu Omosh, amejiunga na chama cha kisiasa cha UDA.

Omosh alivuma sana mitandaoni miezi chache iliyopita baada ya kuomba msaada kutoka kwa wakenya.

Mapema wiki hii muigizaji huyo alivuma sana baada ya kukubali kuuza nyumbani yake kwa milioni 15, huku asijue kwamba ilikuwa utani kutoka kwa mchekeshaji Sleepy David.

Kupitia kwenye picha zilizoenea sana mitandaoni,Omosh anaonekana akiwa amejiunga na chama cha UDA.

Image: Hisani

Chama cha United Democratic Alliance kimetoa taarifa kuhusu ziara ya muigizaji Joseph Kinuthia almaarufu Omosh, katika ofisi zao

Baada ya picha za Omosh kuenea sana mitandaoni akiwa kwenye makao makuu ya chama hicho, wengi walishindwa nini hasa ni ajenda yake.

Katika taarifa ya Katibu Mkuu wa UDA Veronica Maina, alisema kuwa muigizaji amejiunga na chama rasmi

"Katibu Mkuu wa UDA Veronica Maina akimpokea  muigizaji Joseph Kinuthia, anayejulikana kama Omosh kwenye makao makuu ya chama.

Omosh amesajiliwa kama mwanachama wa chama na kuidhinisha mfano wa kiuchumi wa taifa wa Hustler akisema kuwa itainua Wakenya wengi wa kawaida kutokana na umaskini.

Alisema Wakenya wenye bidii ambao hawakuwa na fursa watafaidika na mfano wa kiuchumi wa mapinduzi," UDA Ilisema.

Hizi hapa baadhi ya picha za hafla hiyo;

Image: Hisani
Muigizaji Omosh baada ya kujiunga na chama cha UDA
Image: Hisani