logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Kwa hivyo alitaka niishi kama mti? Nyota Ndogo asema mumewe hajamuacha

Licha ya yake kutozungumza naye alikuwa anamtumia fedha na kumlinda kama mumewe.

image
na Radio Jambo

Habari15 September 2021 - 11:41

Muhtasari


  • Mwimbaji kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliandika wasiwasi wake kuhusu mume wake
  • Nyota alisema kwamba mumewe Hurricane aliamua kwenda kimya juu yake tangu Aprili, lakini alijua  vizuri utamaduni wake wa Kiislam
Nyota Ndogo na mume wake mzungu

Mwimbaji kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliandika wasiwasi wake kuhusu mume wake.

Nyota alisema kwamba mumewe Hurricane aliamua kwenda kimya juu yake tangu Aprili, lakini alijua  vizuri utamaduni wake wa Kiislam.

Licha ya yake kutozungumza naye alikuwa anamtumia fedha na kumlinda kama mumewe.

Hata hivyo, mambo yaligeuka mabaya wakatialipakia picha akiwa na mwanamume mwingine Patrick kama mpenzi wake.

"Haya maisha bwana hayataki hasira kabisa. Yani mimi huyu ameninunia toka April lakini sheria za dini yetu kidogo anazikumbuka

so kwaufupi huyu baba kila mwezi ananitumia hela za matumizi yangu KAMA mke wake japo haongei

Am sorry @officialpday_hurrikane mume wangu amerudi tu baada ya kuona picha zetu tukiwa hoteli tumeshikana mauno na ndio ameleta Sasa zogo na Kusema hajaniwacha na siwezi ku move on kama sijapewa talaka na hajawacha kuniudumia.

Shida yangu mimi ni kunyamaziwa miezi yote. Yani @pday wewe ndio umesababisha huyu mbabaa aongee?," Aliandika Nyota.

 Kulingana na yeye, Nyota Ndogo bado ni mkewe, na ukweli kwamba alikuwa akituma fedha zake ni kuthibitisha kwamba hawakuwa na talaka bado.

"Kwaivyo alitaka niishi kama mti?. SABABU YA MIMI KUWACHA KUPOST PICHA ZAKO VIDEO TULIOFANYA PAMOJA NI KUA HUYU MBABAA AMENIKATAZA.

nitajaribu kuipush kivyengine. Kimimi naona naishi tu kama mti. WAKATI ATAKAPO AMUA KUJA KENYA NDIO NITASEMA NINA MUME KAMILI SAIZI NAONA KAMA 50 50

maana hajasema anakuja ama haji na mimi nimechoka kubembelezana Sasa...... @pday picha zetu na video ndio zimemuuma huyu mume wangu kufunguka. Naskia vibaya Kua nimeshindwa kupost video yetu.. "

Alijiuliza jinsi Hurricane alivyotaka yeye aweze kukaa, maisha bila kuzungumza na bado anadai kwamba ni ke wake.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved