'Sikulala darasani,' Juliani amsifia Lilian Ng'ang'a huku akifichua siku ya kwanza waliopatana

Muhtasari
  • Juliani amsifia Lilian Ng'ang'a huku akifichua siku ya kwanza waliopatana
Lilian Ng'ang'a na Juliani
Image: Boniface Mwangi/Twitter

Ndio wamekuwa wakivuma baada ya kufichua kwamba wawili hao ni wapenzi, na hakuna kitu ambacho watu wanaweza fanya,kwani ulikuwa uamuzi wao.

Msanii Juliani na aliyekuwa mkewe gavana wa Machakos Alfred Mutua, Lilian Ng'ang'a waliweka uhusiano wao hadharani siku chache baada ya Lilian na MUtua kutangaza kutengana kwao huku wakizua mdahalo mitandaoni.

JUliani akiwa kwenye mahojiano na the standard alimlimbikizia LIlian Sifa za kipekee huku akifichua kwamba walikutana Juni mwaka huu.

Msanii huyo  alifichua kwamba alimpenda Lilian mara moja baada ya kukutana na shukrani zake kwa sifa ambazo yeye hubeba.

Juliani alibainisha kuwa alivutiwa na Lilian kwa sababu ya maadili yake, uwazi wa akili na kusudi

"Lilian nilikutana naye mapema Juni au katikati ya Juni. Kama mwanamume, sikulala katika darasa. Sijawaona wanawake wengi kama yeye. Ana ufafanuzi wa akili, uwazi wa kusudi, aina ya vitu anayothamini, kujiheshimu. "Juliani alisema.

Usemi wake JUliani unajiri siku chache baada ya kukana madai kwamba alimuibia mtu mpenzi wake.