'Mke wangu alikuwa anataka nipone haraka,'King Kaka amshukuru mkewe Nana kwa kusimama naye

Muhtasari
  • Wiki chache zilizopita rappa King Kaka, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alifahamisha mashabiki wake amekuwa mgonjwa kwa miezi 3 huku akipoteza kilo 33
  • Pia alifichua kwamba anaendelea vyema kutokana na ugonjwa wake
Msanii King Kaka na mkewe Nana Owiti
Image: Instagram/KIng Kaka

Wiki chache zilizopita rappa King Kaka, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alifahamisha mashabiki wake amekuwa mgonjwa kwa miezi 3 huku akipoteza kilo 33.

Pia alifichua kwamba anaendelea vyema kutokana na ugonjwa wake.

Kupitia video ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, gwiji huyo wa nyimbo za kufoka aliwashukuru sana mashabiki ambao wamekuwa wakimuombea na kumtumia jumbe za kumtakia afueni ya haraka.

"Asante kwa maombi yenu na jumbe zenu na tusiache mazee. Naendelea kupata nafuu, nishatoka hospitali" King Kaka amesema.

Msanii huyo ambaye alikuwa amefichua kuwa alipoteza kilo 33 kufuatia maradhi yaliyomwadhiri kwa miezi mitatu alisema kwamba kwa sasa anaendelea kufuata maagizo ya daktari kuhusiana na lishe.

Siku ya Jumatatu Kaka alimshukuru mkewe kwa kuwa naye na kumpa motisha alipokuwa mgonjwa.

Kulingana na King Kaka mkewe alionyesha kuwa mwanamke, na rafiki ni nini, wakati wa kipindi hicho alichokuwa mgonjwa.

Napenda kuhesabu baraka zangu. Miezi 3 iliyopita hakuwa na kitu cha muda mfupi lakini cha kutisha, mwanamke huyu hapa @nanowiti ameonyesha na kuthibitishwa nini mke na rafiki bora ni.

"Kutoka Kulala Kwakiti cha Hospitali karibu na kitanda changu basi wewe kuamka oga katika hospitali hiyo, kwenda na kutabsamu kwa runina  kama kila kitu ni sawa kupigana na wauguzi kwa nini wao wanfanya kazi polepole (asante kwa wauguzi ambao walinitunza, ni vile Nana alikuwa anataka nipone haraka) Kuomba na kunitia moyo ni kule

Kuteremsha presha yangu nilipokuwa na joto jingi mwilini, sasa niko katika hatua ya kupona lakini naomba Mungu akutumizie mahitaji ya moyo wako

Nimejifunza neno jipya na maana ya mwenzi katika uhusiano,barikiwa na asante Nana," Aliandika Kaka.