Ringtone apewa nafasi ya kutatua shida ya hakimiliki ya kibao chake na Rose Muhando la sivyo kitolewe Youtube

Muhtasari
  • Ringtone apewa nafasi ya kutatua shida ya hakimiliki ya kibao chake na Rose Muhando la sivyo kitolewe Youtube
ringtone apoko
ringtone apoko

Msanii Ringtone ni mmoja wa wasanii wa kiume ambao wamesalia katika tasnia ya nyimbo za injili kenya.

Msanii huyo anafahamika kwa kutafuta kiki, kutoka kwa mashabiki wake kwa sababu moja au nyingine. lakini licha ya hayo yote amekuwa akizingatia kazi yake.

Ringtone ametoa vibao, huku akiwa amewashirikisha wasanii tofauti ikiwemo Rose Muhando.

Kwenye ukurasa wake wake instagram Ringtone amefichua kwamba amepewa siku saba atatue shida ya hakimiliki ya kibao chake cha 'Yesu angare'.

KUlingana na habari kutoka Youtube msanii mmoja amewashataki kwa kutumia hakimiliki yake.

Hata hivyo youtube ilimfahamisha Ringtone asipozungumza na kutatua shida hiyo kibao chake kitatolewe kwenye mitandao ya youtube.

"Kuna msanii wa nyimbo za injili amedai kwamba kuna shida ya akimiliki, katika kibao changu na Rose Muhando, wanataka kufuta kibao cha 'Yesu Angare kutoka youtube," Aliandika Ringtone.

Hizi hapa hisia za mashabiki;

eddwincosmas: Let delete song not singing good is you😢 fair it's not 😂

sultanmayakaI:  wanna email her, awache upuzi or nitamfinya

gachuhiw: Yes,is you is delete them together with Rose muhando

youngblood_rigol: Sad yo rose muhando cry