Niombeeni badala ya kutaka nizae mtoto wangu mapema-Vera Sidika

Muhtasari
  • Kulingana na Vera hakuna haja ya kuaharikisha kujifungua na hana shida yeyote, huku akiongeza kwamba watu wengi wamejifungua mapema lakini haikuwa matakwa yao
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti na mama mtarajiwa Vera Sidika,amewakasirikia baadhi ya mashabiki wake mitandaoni ambao wamekuwa wakimtumia jumbe kuwa anapaswa kujifungua mtoto wake kabla ya muda kufika.

Kulingana na Vera hakuna haja ya kuaharikisha kujifungua na hana shida yeyote, huku akiongeza kwamba watu wengi wamejifungua mapema lakini haikuwa matakwa yao.

"Hakuna mtu aliyesema huwezi kuwa na mtoto kabla ya muda. Inatokea dhidi ya mapenzi yao, hakuna mtu angeweza kutembea katika hospitali na kusema  wanataka kuwa na mtoto wao kwa wiki 30 au kabla ya muda

Kwa sababu DMS nyingi zinasema kuwa nilikuwa na mtoto wangu kwa wiki 25 kwa wiki 33 nk na walikuja vizuri

Kisha ninawauliza na kusema haikuwa kwa uchaguzi. Kwa nini ninyi nyote mnataka nijifungue maema kabla wakati na muda wangu haujafika,ilhali sina shida yeyote mnapaswa kuomba kwa ajili ya afya na kujifungua vyema."

Vera aliwatakia akina mama wote ambao wnasubiria kujifungua, wajifungue vyema.