'Tayari najua mwanamume ambaye atanioa,'Saumu Mbuvi azungumzia kuolewa tena

Muhtasari
  • Saumu Mbuvi azungumzia kuolewa tena
  • Mapema mwaka huu Anwara na Saumu waliachana licha yao kubarikiwa na mtoto mmoja.
Saumu Mbuvi
Image: Studio

Saumu Mbuvi, alivuma mitanaoni baada ya kuachana na seneta Anwar, na kudai kwamba amekuwa akimdhulumu katika ndoa yake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, sekta ya Q&A alifichua kwamba anatazamia kuolewa, sio kuolewa tu bali alisema kwamba anamjua mwanamume ambaye atamuoa.

"Je unatazamia kuolewa tea," Shabiki aliuliza.

"Ndio pia najua yule atanioa tayari," Alijibu Saumu.

Saumu yuko Dubai kwa harakati za kibiasara, akizungumzia hayo alisema kwamba  hana furaha kwani ni mara yake ya kwanza kuwa mbali na watoto wake.

"Kwa sasa sina furaha,  i mara yangu ya kwanza kuwa mbali na watoto na familia yangu."

Mapema mwaka huu Anwara na Saumu waliachana licha yao kubarikiwa na mtoto mmoja.