Wakenya wastaajabu baada ya mfanyibiashara mwanamke kutunuku mwanawe wa miaka 6 jumba la kifahari akiadhimisha siku ya kuzaliwa

Muhtasari

•Bi Maluli alisema kwamba alichukua hatua ya kununua jumba hilo la mamilioni ya pesa ili kutimiza ahadi ambayo alikuwa amempatia mwanawe  na kudai kwamba mtoto huyo ndiye mmiliki rasmi.

Jumba la Bayden
Jumba la Bayden
Image: INSTAGRAM// MERCY MALULI

Mwanamke mmoja mfanyibiashara mahuhuri jijini Nairobi amewaacha wanamitandao wengi vinywa wazi baada ya kununulia mwanawe jumba kubwa kama zawadi ya kuadhimisha kutimiza miaka 6.

Mercy Maluli ambaye anamiliki duka la kuuza nguo la Divine Collections alimtunuku Brayden jumba lenye ghorofa tatu akidai kwamba mwanawe amekuwa akitamani sana kupata nyumba.

Bi Maluli alisema kwamba alichukua hatua ya kununua jumba hilo la mamilioni ya pesa ili kutimiza ahadi ambayo alikuwa amempatia mwanawe  na kudai kwamba mtoto huyo ndiye mmiliki rasmi.

"Amekuwa akiomba sana apate nyumba kwa kuwa mamake alimuahidi kumnunulia moja. Mungu amejibu maombi yake na sasa yeye ndiye mmiliki wa nyumba mpya jijini" Ni Maluli aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha za jumba hilo maridadi lililokuwa limepambwa na baluni na kuashiria kwamba lilikuwa zawadi la kuadhisha siku ya kuzaliwa.

Mbenyenye huyo alisema kwamba mwanawe humpa raha kubwa moyoni na ako tayari kupatia watoto wake chochote wanachohitaji.

"Chochote kwa wavulana wangu, siku angavu mbeleni.. analeta raha kubwa maishani mwangu. Singeifanya kwa namna ingine" Maluli alisema.

Wanamitandao wengi wameshangazwa na hatua ya Maluli kuona kuwa mwanawe ako na miaka 

@alex_mwakideu You bought him a house on his sixth birthday! Please adopt me @mercy_maluli.. And Happy Birthday to your boy. More blessing to you and your family

@squiro: You bought him a house at 6 Mimi mama yangu alinipea mattress nianze maisha nayo after form 4😢😢😢

@oficial_v.incenti also want to be adopted😂

Maluli alimshukuru Mungu kwa zawadi ya mwanawe ambaye alisema kwamba ni mshirika wake katika maombi.