Kwa nini sikumpa ujauzito Vera sidika- Chansa azungumza

Muhtasari
  • Mpenzi wa zamani wa Vera Sidika Jimmy Chansa anasema wakati alikuwa kwenye uhusiano na sosholaiti wa Kenya, hakuweka kipaumbele kupata mtoto

Mpenzi wa zamani wa Vera Sidika Jimmy Chansa anasema wakati alikuwa kwenye uhusiano na sosholaiti wa Kenya, hakuweka kipaumbele kupata mtoto.

Alipoulizwa kwa nini hakutaka kumpa ujauzito Sidika, alisema;

"Kila mtu ana chaguo ambalo ni nani angependa kupata mtoto naye. Mtoto ni baraka kubwa. Ikiwa una kitu mikononi mwako na ukiachilie, inamaanisha ilikuwa imepangwa kuwa hivyo."

Aliomgeza kuwa;

"Hakuna anayenipenda kuliko vile ninavyojipenda mwenyewe. Ni sawa kuachana na mtu kisha mtu huyo apate mtoto na mtu mwingine. Hilo ni chaguo lao."

Aliendelea kusema kuwa anaweza kupata mtoto na mwanamke ikiwa anataka.

"Ikiwa ninataka mtoto, nitampata."

"Kuna watu bilioni nane ulimwenguni na sio wakati wangu wa kupata mtoto. Mungu ndiye anayewapa watoto.

Kwangu kupata mtoto sio kipaumbele kwa sasa. Ikiwa wakati utafika, kuna takriban wanawake bilioni nne katika dunia."