'Kiki za kifala sana,'Mashabiki wamwambia msanii B Classic baada ya kudai ameacha muziki

Muhtasari
  • Msanii B Classic ashambuliwa na mashabiki baada ya kudai anaacha muziki
Msanii B Classic
Image: Studio

Msanii kutoka kaunti ya Taita Taveta B Classic ni miongoni mwa wasanii chipukizi, ambao wamekuwa wakitia bidii katika kazi yao ya usanii kila kuchao.

B Classic ametoa vibao kadhaa ambavyo vimependwa na mashabiki mitandaoni.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, msanii huyo amedai kwamba  amewacha muziki kwani hajakuwa akishikwa mkono na mashabiki.

Msshabiki wengi hawajachukulia haya kama jambo la kushangaza bali asilimia kubwa wamedai kwamba ni kiki tu, kama vile wasanii wengine wamekuwa wakitafuta ili kutoa kibao kipya.

"Nimeacha muziki 😰 Kwa sababu ya kuchanganyikiwa, hakuna msaada kutoka kwa mashabiki 😰sijawahi fikiria kama ningechoka na kitu nakipenda  hali ya Ila itawahimiza, kwa wale ambao waliamini poleni Labda siku moja mambo inaweza kubadilika. Bahati nzuri kwa hustle yangu mpya 😰😰😰," Aliandika B Classic.

KUlingana na video aliopakia kwenye ukurasa wake wa instagrama msanii huyo amedai kwamba amerudi kufanya kazi ya kutengeneza magari.

Mashabiki walikuwa na haya ya kusema;

baddi_money....: kiki za kifala sanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

alex_karisa: mbona hupatikani kwa simu , usichoke mwana

seggyyusta: Ndima ni ndima, Bora kibala..

mwendwaamjukuu: KikiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

ondijo076: Hii ngoma inatoka liniπŸ”₯

presenter_ali: Mwana Rudi bana tupige shughuli , usifanye hivyoo

mathew.alfred.1694: Naamn hiii bonge la song

lilmad._: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚bro ambia watu ukweli...