Nimefika mwisho!Naiboi asema huku akifichua hawezi toa nyimbo zaidi ya 800

Muhtasari
  • Msanii  Naiboi ameomba maombi kutoka kwa mashabiki wake,Naiboi anasema amekuwa akiweka vitu kwake lakini hawezi tena
  • Msanii huyo amesema licha ya kuwa na nyimbo zaidi 800, hawezi toa ata moja
naiboi
naiboi

Msanii  Naiboi ameomba maombi kutoka kwa mashabiki wake,Naiboi anasema amekuwa akiweka vitu kwake lakini hawezi tena.

Msanii huyo amesema licha ya kuwa na nyimbo zaidi 800, hawezi toa ata moja.

Pia hakufichua sababu za kutotoa muziki wake, kwani ni miongoni mwa wasanii ambao wanafahamika sana Afrika Mashariki na ulimwenguni kote.

"Nilichotaka ni kutoa muziki kwa mashabiki wangu. Na mafahamu wa najua wana shanga kuna nini na Naiboi !! Mikono yangu imefungwa kwa karibu miaka miwili Sasa.

Na nimechoka kuwa na huruma ya hawa wasee. Ningehitaji wanasheria wazito. Nimefika mwisho. Nimemkumbuka NaiBoi kama wewe. Niombee. Ninaweka kila kitu kwangu sana.

Lakini imefika mwisho. Ninaupenda muziki sana inaniuma nina nyimbo zaidi ya 800 na siwezi kutoa hata moja ??????????," Aliandika Naiboi.

Kwa kuangalia kwa vitu, Naiboi anaweza kuwa na tatizo na usimamizi wake.

Katika matukio mengine, usimamizi unaweza kumkataza msanii haki ya kutoa nyimbo kulingana na hali ya mkataba waliyoifanya.