"Ndio tulichumbiana" Mwigizaji Lenana Kariba athibitisha uhusiano wake na Betty Kyalo

Muhtasari

•Kariba ambaye anatambulika sana kutoka kwa kipindi 'Auntie Boss' na 'Selina' ambapo aliigiza kama Lionel na Reagan mtawalia alithibitisha uhusiano wake na Kyallo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

•Mnamo mwezi Septemba Kariba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake mzungu kutoka Uholanzi katika visiwa vya Carribean.

Image: INSTAGRAM

Orodha ya watu mashuhuri ambao wamewahi kuwa na uhusiano na mwanahabari Betty Kyalo inaendelea kuongezeka huku mwigizaji Lenana Kariba sasa akithibitisha kuwa aliwahi kuwa na uhusiano naye.

Kariba ambaye anatambulika sana kutoka kwa kipindi 'Auntie Boss' na 'Selina' ambapo aliigiza kama Lionel na Reagan mtawalia alithibitisha uhusiano wake na Kyallo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Alipokuwa anashirikisha mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu, shabiki mmoja alitaka kubaini iwapo madai kuwa mwigizaji huyo amewahi kuchumbiana na Kyallo ni ya kweli.

"Ndio tulichumbiana kitambo sana tukiwa wadogo" Kariba alijibu huku akiambatanisha jibu lake na picha ya kumbukumbu ambayo walikuwa wamepigwa pamoja katika enzi zile.

Hata hivyo mwigizaji huyo hakuthibitisha walichumbiana mwaka gani wala kwa kipindi cha muda gani.

Image: INSTAGRAM// LENANA KARIBA

Mnamo mwezi Septemba Kariba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake mzungu kutoka Uholanzi katika visiwa vya Carribean.

Kariba na Hellen wamekuwa pamoja kwa muda na kwa sasa wanaishi nchini Uingereza baada ya kufunga  ndoa.

Kwa sasa inaaminika kuwa Betty Kyalo ako kwenye mahusiano na wakili mashuhuri Nick Ndeda ambaye wamekuwa wakionekana pamoja sana mitandaoni tangu mwezi Julai.

Hapo awali mtangazaji huyo amewahi kuhusishwa na Dennis Okari na gavana mmoja mashuhuri nchini .