"Nikikufa wauguzi hawatashika sehemu zangu za siri!" Mhubiri James Ng'ang'a aapa

Muhtasari

•Kwenye video ambayo imesambazwa sana mitandaoni Ng'ang'a anasikika akitoa onyo kali kwa wahudumu wa afya kwamba wasidhubutu kushika sehemu zake za siri atakapofariki.

•Mtumishi huyo wa Mungu aliapa kuwa hata wakati atakopokuwa maiti hatastahimili uume wake kukejeliwa na wauguzi.

Askofu David Ng'ang'a
Askofu David Ng'ang'a
Image: IVY MUTHONI

Miaka nenda miaka  rudi mhubiri mashuhuri nchini James Maina Nga'ng'a ameendelea kushangaza Wakenya na utata mkubwa ambao umezingira taaluma yake.

Mwazilishi huyo wa kanisa la Neno Evangelism Center anajulikana  kufanya matendo ya kustaajabisha ama kutoa matamshi tatanishi hadharani bila woga wowote.

Hivi majuzi mhubiri huyo alipokuwa anaendeleza ibada kanisani mwake alitangaza wazi jambo moja ambalo angependa lisifanyike wakati safari yake duniani itafika hatima.

Kwenye video ambayo imesambazwa sana mitandaoni Ng'ang'a anasikika akitoa onyo kali kwa wahudumu wa afya kwamba wasidhubutu kushika sehemu zake za siri atakapofariki.

"Mimi siku yangu nikiondoka naamini Mungu wangu, hawa wasichana wauguzi hawatashika sehemu zangu za siri eti njoo uone Ng'ang'a" Ng'ang'a alisema akiwa kwenye jukwaa la kanisa.

Mtumishi huyo wa Mungu aliapa kuwa hata wakati atakopokuwa maiti hatastahimili uume wake kukejeliwa na wauguzi.

"Watoto hawa wadogo hawawezi  enda kushikashika sehemu zangu za siri. Eti hebu njoo uone Ng'ang'a, kumbe huwa ana uume mkubwa hivi. Watoto wadogo hawa, mtumishi wa Mungu.. inawezekana kweli?" Ng'ang'a aliapa.

Ng'ang' a aliomba sana asipatwe na aibu wakati wa kifo chake utakapowadia.

Wiki chache zilizopita mhubiri huyo aliwaacha wengi na mshangao baada ya kudai kuwa ako na watoto zaidi ya 70 kote nchini.

Kwenye video ambayo ilienezwa sana mitandaoni, Ng'ang'a alisikika akifichulia waumini katika kanisa lake kwamba ana makumi ya watoto katika maeneo mbalimbali nchini.

"Mimi huwa naambia watu niko na watoto kama sabini hivi. Ukambani kama 30, Ukienda Mombasa kama ishirini na kitu hivi, huko Murang'a  na Nyandarua" Ng'anga alidai.

Ng'ang'a alidai kwamba alifanya majaribio mengi ya ndoa ila hakuwa anapata mafanikio kwani kila alipojaribu alikuwa anajipata akitengana nao baada ya muda ama kitu kingine kutokea na kufanya uhusiano ufikie kikomo.

"Mwingine alienda akiwa na ujauzito wa miezi sita. Alisema ameenda kuchua nguo lakini hakurudi" Ng'anga alisema.