Mauzo amtunuku Vera Sidika shamba Watamu anapotayarisha kujifungua hivi karibuni

Muhtasari

•Mauzo alisema kuwa aliamua kuzawadi kipenzi chake shamba upande wa watamu kwani anapendelea sana kuenda likizo katika eneo hilo la Malindi.

•Wazazi hao watarajiwa  tayari wametangaza kuwa wakati wowote sasa wanatarajia kukaribisha binti yao ulimwenguni.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika ameonekana kuendelea kuvuna makubwa kutokana na ndoa yake na mwanamuziki Brown Mauzo licha ya baadhi ya wanamitandao kutilia shaka uhusiano huo.

Mnamo siku ya Jumapili mwanamuziki Brown Mauzo alisherehekea mkewe kwa kumpatia zawadi ya shamba iliyo katika eneo la Watamu kaunti ya Kilifi.

Video ambayo ilirekodiwa kwenye hafla ya kusherehekea  matayarisho ya kujifungua mtoto maarufu kama 'baby shower'  ilionyesha Mauzo akimkabidhi mke wake mjamzito hatimiliki ya shamba ambalo alikuwa amemnunulia.

Mauzo alisema kuwa aliamua kuzawadi kipenzi chake shamba upande wa watamu kwani anapendelea sana kuenda likizo katika eneo hilo la Malindi.

"Kila wakati huwa ananiambia tuende Watamu, huwa anahisi ako sawa ametulia. Niliona mara nyingi tukifika kule huwa tunaingia kwa nyumba tunatulia. Nikaonelea ni muhimu apate kasehemu kadogo ambapo tutajenga siku za usoni" Mauzo alisema.

Vera alishangazwa sana na zawadi ambayo mumewe alimua kumpatia na kusema kuwa yeye ni kila kitu ambacho aliomba kupata.

Alisema kuwa alipendezwa sana na ile zawadi kwani mara nyingi eneo la Malindi huwa chaguo lake kila anapotaka kuenda likizo.

"Angalia kile @brownmauzo254  amenizawadi!! Weeh, jinsi napenda Malindi/Watamu waah.. Kila tunapotaka kuenda likizo kidogo huko ndiko huwa chaguo letu. Sijjui nilichofanya kustahili  mume huyu. Huwa anafanya zaidi kunifanya nifurahi. Furaha yangu huwa  kipaumbele chake. Nakupenda sana" Vera alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Vera alisema kuwa shamba hilo ni utajiri wa kizazi na kudai kwamba ana imani kubwa kuwa watoto ambao anatarajia kupata na mume wake watakuwa na maisha mazuri.

Sijui nahisi vipi leo. Leo ni siku nyingine ambapo nahisi kulia. @BrownMauzo wewe ni kila kitu niliomba na zaidi. Ulinifanya niamini kuwa Mungu hujibu maombi. Unaweza kuvunjwa moyo mara kadhaa lakini bado upate mtu mmoja maalum ambaye ataishi nawe milele. Mungu akubariki kwa yale umefanyia familia yetu mpya.. utajiri wa kizazi. Zawasi nzuri sana! Najua watoto wetu watakuwa na maisha mema Inshallah" Alisema Vera.

Wazazi hao watarajiwa  tayari wametangaza kuwa wakati wowote sasa wanatarajia kukaribisha binti yao ulimwenguni.

"Mtoto mrembo wa kike ako njiani kuja kutupatia mapenzi yasiyoisha, wakati wowote kutoka sasa.  Mtoto wetu mpendwa, maisha ni safari nzuri na natumai utaishuhudia vizuri! Tafuta bahati, kicheko, matumaini na ufurahi kila siku!" Vera Sidika alimwandikia bintiye mtarajiwa kupitia ukurasa wake wa Instagram.