Mume wa mtu naye kufanywa sponsor ni Kawaida-Msanii Lulu Diva asema

Muhtasari
  • Akiwa kwenye mahojiano Lulu alisema kwamba karne hii ya sasa ni kawaida mume wa mtu kufanywa sponsor
Lulu Diva 'Kama Msanii nimepambana sana kufikia nilipo'
Lulu Diva 'Kama Msanii nimepambana sana kufikia nilipo'

Msanii Lulu Diva, alivuma sana baada ya madai kwamba ndiye alikuwa sababu kuu ya Diamond na Tanasha kuachana, lakini alijitokeza na kukana madai hayo, na kuweka wazi kwamba sio mpenzi wake Diamond.

Si hayo tu pia alivuma baada ya madai kwamba mbunge na msanii Jaguar anamwinda, pia aliakana uvumi huo na kusema kwamba ni marafiki.

Akiwa kwenye mahojiano Lulu alisema kwamba karne hii ya sasa ni kawaida mume wa mtu kufanywa sponsor.

"Kwani We Ujawahi Kusikia Mtu Kachukulia Bwana ?...Mume wa mtu naye kufanywa sponsor ni Kawaida

Hili limekuwa la kawaida katika maisha yetu ya  kila siku, ni mara yako ya kwanza kuskia kuwa mwanamke amenyanganywa mume, au mwanamke amechukua mume wa mtu?" Alisema Lulu.