Upendo unapaswa kukujenga na sio kukuua-Lilian Ng'ang'a asema

Muhtasari
  • Wapenda mchezo wa riadha wanazidi kuomboleza kifo cha Agnes Tirop, ambaye alipataikana ameuawa nyumbani kwake Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet mapema wiki hii
Lilian Ng'ang'a
Image: IINSTAGRAM/LILIAN

Wapenda mchezo wa riadha wanazidi kuomboleza kifo cha Agnes Tirop, ambaye alipataikana ameuawa nyumbani kwake Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet mapema wiki hii.

Wanamitandao,viongozi na watu mashuhuri walilaani kitendo hicho huku weng wao wakiwashauri wanamitandao na mashabiki dhidi ya kukaa kwenye mauhusiaono yenye vurugu.

Katika ujumbe wake Rais Uhuru Kenyatta wa kuomboleza Aganes aliwasihi polisi wachunguze kifo chake na kuwakamata waliohusika.

Siku ya Alhamisi mumewe Agnes alikamatwa na polisi wa Mombasa, na kutiwa mbaroni huku uchunguzi ukiendelea.

Aliyekuwa mkewe gavana wa kaunti ya Machako Alfred Mutua , Lilian Ng'ang'a alilaani kitendo hicho huku akisema kwamba upendo ni wa kukuza mtu na wala sio kumuua wala kumvunja.

Pia alisisitiza kwamba watu wanapaswa kuzungumzia juu ya vurugu katika uhusiano wao, kwani wengi wamepoteza maisha yao kutokana na vurugu na unyanyasaji wa nyumbani.

"Vurugu za ndani zimedai maisha mengi na tunapaswa wote kuzungumza juu yake. Vurugu ya aina yoyote katika mahusiano haipaswi kamwe kuvumiliwa

Upendo ni maana ya kukujenga, si kuvunja na kukuua. Ninasema toka kwenye uhusiano kama huo, jua litafufuliwa tena na muhimu zaidi ni kwamba utakuwa hai ili kufurahia joto.

Kupitia ofisi ya kaunti ya, Machakos, kama moja ya mipango yangu, nilikubaliana na fedha zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha GBV. Kituo cha GBV, mara moja kikikamilika, kitakuwa salama kwa washindi wa unyanyasaji wa ndani," Aliandika Lilian.

Usemi wake unajiri wakati familia ya Agnes Tirop inadai haki kutendeka kwa mwana wao.