'Milly Wajesus hakumpa mtu ujauzito,'Sarah Kabu amwambia Edgar Obare

Muhtasari
  • Sarah Kabu, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemwambia mwanablogu Edgar Obare amuache Milly Wajesus
kabi
kabi

Sarah Kabu, kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemwambia mwanablogu Edgar Obare amuache Milly Wajesus.

Hii ni baada ya wanamitandao kutoa hisia tofauti kuhusu Milly Wajesus na Kabi Wajesu, baada yao kusafiri kuenda Turkey.

Kulingana na mwanamtandao aliyetangulia kumwandikia mwanablogu Edgar Obare, alilalamikia familia ya Wajesus waliokuwa wakisafiri kuwaacha mtoto wao, Taji Wajesus na yaya.

Aliendelea kudai kuwa Kabi Wajesus ametelekeza mtoto wake na baby mama wake ambapo anadai wanapaswa pia kuwapa taarifa wanamtandao jinsi wanavyomsaidia mtoto wao badala ya kusambaza video zao wakisafiri nje ya nchi.

Sarah Kabu alikerwa na ujumbe wake Edgar na kuipakia tena akimtaka aiache familia ya Wajesus peke yake.

Pia amemtaka Edgar kuacha kumsumbua Milly Wajesus kwa sababu yeye sio wa kulaumiwa.

Aliendelea kumwomba baby mama wa Kabi pia afanye kazi kwa bidii na kumtunza mtoto wake badala ya kuwalaumu Kabi na Milly kwa kushindwa kwake.

"Mko wapi njoo unisaidie Kushauri @millywajesus jinsi ya kukabiliana na mchezo wa kuigiza wa baby mama ambaye anahisi kuwa ana haki?

Weuh... sasa sijui Edgar anataka kuwa wanabaki pamoja @kabiwajesus akisafiri ama watoto wanatetewa ili wasafiripamoja na wake?

Nafkiri kila mtu ashikamane mipaka yao ukitaka likizo tutakupanga  bora ROI lakini heshimu mume wake kwani huwa anasaidia mtoto wako. sio wako tena ukiachwa achika na usifikie jasho la mama mwenzako kwa jina la usaidizi wa mtoto sasa wewe ni brand pia jisort. mos mos," Aliaka Sarah.

Wanamtandao waliendelea kuitikia chapisho la Sarah Kabu lakini alirudia tena kuwataka wapeleke maoni yao kwa Edgar Obare kwa sababu hakuwa akinunua maoni yoyote.

"Edgar wachana na Milly yeye hakumpa mtu mimba Ni wanawake wangapi wanasafiri kwaajili ya biashara bila watoto? Unatarajiaje kwenda kufanya manunuzi nje ya nchi chini ya jiji na mtoto katika enzi hii ya corosh."