Nilipoambiwa kuhusu kifo cha mume wangu,sikufikiria kuhusu mwanangu-Ruth Matete

Muhtasari
  • Baada ya kupokea habari ya kifo cha mumewe, Ruth anasema alisahau kuhusu mtoto wake kwa muda mfupi
ruthmatete
ruthmatete

Msanii wa nyimbo za injili Ruth Matete amefunguka kuhusu  kumpoteza mumewe wakati alipokuwa na ujauzito wa kifungua mimba wake.

Katika mahojiano  Ruth Matete alisema kuwa ajali ya moto ilitokea wiki 1 baada ya kutambua kwamba alikuwa mjamzito.

Baada ya kupokea habari ya kifo cha mumewe, Ruth anasema alisahau kuhusu mtoto wake kwa muda mfupi.

"Nilipoambiwa kwamba mume wangu ameaga dunia, sikuwahi kufikiria kuhusu mtoto wangu. Huyu ni mume wangu, tulikuwa tumeoana tu kwa miezi minne, upendo wa maisha yangu, mtu nilitaka kuuishi maisha yangu naye

Kuwa mwaminifu, sikufikiri juu ya mtoto, ujauzito, sikujali kama nilipoteza. Wakati huo nilikuwa nikiomboleza

Nilikubali tu kwa huzuni, nilihitaji kukubali. "

 Hata hivyo, alianza kumtunza mtoto kwa kutambua kwamba kumbukumbu za mumewe ziko ndani ya mtoto wake.

Ruth anasema mumewe alikufa wiki tu baada ya kufahamu alikuwa  mjamzito.

"Tulipata tu tulikuwa tunatarajia wiki moja kabla ya ajali kutokea. Tulinunua gesi na silinda na ilikuwa ni kosa." Alisema.