Mwanamuziki Omah Lay azungumza kuhusu uvumi kuwa anachumbia Tanasha Donna

Muhtasari

•Alipokuwa kwenye mahojiano baada ya kutua nchini siku, mwanamuziki huyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba.

•Kumekuwa na uvumi kuwa mwanamuziki huyo amejaza nafasi iliyoachwa na Diamond zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya video iliyoonyesha wakijiburudisha pamoja kuenezwa mitandaoni  wiki kadhaa zilizopita.

Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Omah Lay kutoka Nigeria amefutilia mbali uvumi kuwa anachumbia aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platnumz, mwanamuziki Tanasha Donna.

Alipokuwa kwenye mahojiano baada ya kutua nchini siku, mwanamuziki huyo aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mchumba.

Hata hivyo staa huyo wa muziki alifichua kuwa aliwahi kuwa na mpenzi kutoka Kenya ila hakutaja jina la mwanadada aliyekuwa anachumbia.

"Sina mchumba. Niliwahi kuwa na mpenzi kutoka Kenya lakini sasa niko single! Sitaki kuzungumza kuhusu uvumi huo kutoka Instagram, zile video na zinginezo kwenye mtandao wa Instagram" Omah Lay alisema.

Kumekuwa na uvumi kuwa mwanamuziki huyo amejaza nafasi iliyoachwa na Diamond zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya video iliyoonyesha wakijiburudisha pamoja kuenezwa mitandaoni  wiki kadhaa zilizopita.

Wanamuziki hao wawili walionekana pamoja wakati Omah Lay alikuwa anafanya tamasha katika nchi jirani ya Sudan Kusini.

Siku ya Jumamosi na Jumapili Omah Lay alitumbuiza mashabiki wake  katika hoteli ya Royal Gardenia Gardens Evergreen.