'Nilidanganya nilikuwa mjamzito,ataachwa tu,'Shakilla amshambulia Miss P

Muhtasari
  • Kulingana na Shakilla, pia naye alidanganya kuwa na ujauzito awali ilhali hakuwa na ujauzito wowote

Mwanasholaiti chipukizi Shakilla, kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram, amefutilia mbali madai kwamba Eric Omondi amempachika msanii Miss P ujauzito.

Kulingana na Shakilla, pia naye alidanganya kuwa na ujauzito awali ilhali hakuwa na ujauzito wowote.

Huku baada ya kufunguka aliendelea kumkejeli Miss P, kwa kutokuwa makini, kuwadanganya mashabiki.

Shakilla alimwambia Miss P wakati mwingine aweze kumuajiri mhariri mzuri ambaye anajua kazi vyema, kwani ujauzito wake haukuwa umechorwa vizuri.

"Kwanza ilikuwa ni mimi ambaye nilidanganya kwamba nina ujauzito wa malkia wao,baada ya kufanya hayo mara nyingi ili video iwe njema alafu naona picha ya msichana ambayo haijaharriwa vyema akisema amechukuliwa

Wakati mwingine ni afadhali ununue kivimbe cha mtoto,ama upate mhariri mzuri, kuwajibika kitu gani, mwambie atatumiwa na kisha aachwe baada ya video uoata watazamaji wengi," Alisema Shakilla.

Katika chapisho nyingine Shakilla alimkejelli Eric Omondi, kwa kusema kwamba atawajibika, huku akishindwa kwani hakuogopa kufunga goli mahali kila mtu alikuwa anafunga.

"Hauogopi kufunga mahali mwanamume mwingine alifunga kupia free kick, na kila goli ambazo ziko ili sisi tujue kwamba huwa anaimba

Niliimba 'sunday school' na hamna mtu yeyote alikuwa hapo wa kunisaidia, lakini kwa nini najisumbua hawezi fikia wasanii wa kenya."