'Umemuanika kama nguo baridi,'Cate Maribe ampongeza Jacque kwa kumuanika Eric Omondi

Muhtasari
  • Jacque aliweka wazi uhusiano wake na Eric uko sawa ilhali hawajibikii mahitaji ya mtoto wake
Jacque Maribe
Jacque Maribe

Mchekeshaji Eric amekuwa gumzo mitandaoni kwa muda mrefu sasa, hii ni baada ya kudai kumpachika Miss P ujauzito.

Akiwa kwenye mahojiano Eric Omondi alianikwa na baba mama wake Jacque Maribe kwa kutowajibika na kumtunza mwanawe.

Jacque aliweka wazi uhusiano wake na Eric uko sawa ilhali hawajibikii mahitaji ya mtoto wake.

Baada ya Jacque kumuanika Eric, dada yake Cate Maribe alimpongeza kwa kufichua Eric na kumuonya kwamba hawezi kumtimia mwanawe kutafuta kiki.

"@Ericomondi sasa umefichulia,kumpigia dada yangu ukiwa kwenye mahojiano, ukifikira atacheza na wewe @jacquemaribe umemuanika kama nguo baridi kwa fence ya sengenge

Kazi mzuri mama,usimtumia mtoto wako kutafuta kikibaa ni ule analea si ule wa sperm donor.PS nangoja umalize kupark gari unitumie karo ya mtoto..lakini pole ulikuwa mwaka jana."