Wajibika-Sarah Kabu amwambia Eric Omondi

Muhtasari
  • Pia Maribe, alifichua kwamba hajui mara ya mwishi ya mchekeshaji huyo kuona mwanawe,wala hajawahi mlipia karo
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Eric Omondi atafanya chochote kutafuta kiki ili avume kwa muda mitandaoni, siku ya JUmatatu Eric aliwashangaza wanamitandao baada ya kudai kumpachika Miss P ujauzito.

Kulingana na wanamitandao ERic na Miss P wanatafuta tu kiki, ilhali alkiwa kwenye mahojiano na Mungai Eve alikana madai hayo, na kusisitiza kwamba ujauzito huo ni wake.

Lakini kwa maoni yako ni kiki tu au ni ukweli?

Maoni yaliyotiliwa maanani, ni pale Eric alisema kwamba atawajibika, huku baby mama wake Jacque Maribe akisema kwamba hajakuwa akiwajibika kwa miaka 7.

Pia Maribe, alifichua kwamba hajui mara ya mwishi ya mchekeshaji huyo kuona mwanawe,wala hajawahi mlipia karo.

Kwanini umeamua kufichua siri hii baada ya miaka hiyo yote? Maribe aliulizwa.

"Kwa sababu nilikuwa na kulinda na kwa ajili ya mtoto wetu, lakini unapaswa kuwajibika kama baba ya mtoto wako, ata hujui mwisho wa kuongea naye wala kumuona, wewe ni deadbeat," Maribe alizungumza.

Sarah Kabu, alisikitishwa na vitendo vya Eric, na kumshauri kwamba anapaswa kuwajibika.

Pia alimwambia kwamba anapokea pesa nzuri kutokana na ucheshi wake na wala haoni sabau ya kuto msaidia mwanawe.

"@ericomondi wewe ni rafiki yangu mzuri na pia ni shabiki wako mkubwa pia! lakini kutolipa karo ya shule na kumtunza mtoto wako na kuifanyia mzaha moja kwa moja kwenye kamera si jambo la kuchekesha hata kidogo.

Nimevunjika moyo kwa ajili ya Jackie tafadhali kuwa mwanamume na wajibika kwani najua unatengeneza pesa nzuri na vichekesho vyako. Tunaishi katika nyakati ngumu bana," Sarh Kabu alimshauri Eric.

Haya wadau sijui tumpeleke Eric Omondi kwenye kitengo cha Deadbeat, na mtangazaji Massawe au vipi?