Wakosanao ndio wapendanao! Eric Omondi na Maribe waomba msamaha na kukubaliana kushirikiana katika ulezi

Muhtasari

•Wawili hao waliletwa pamoja na mjasiriamali mashuhuri Simon Kabu siku ya Alhamisi na wakawa na maafikiano mazuri.

•Wawili wao walikubaliana kwamba mtoto ni wao wote na kuahidi kuwa wako tayari  kushirikiana katika ulezi.

Jackie Maribe na Eric Omondi walipopatana siku ya Alhamisi
Jackie Maribe na Eric Omondi walipopatana siku ya Alhamisi
Image: SIMON KABU

Hatimaye  Eric Omondi na mwenzake Jackie Maribe ambao hivi karibuni wamekuwa wakitumbuiza wanamitandao na drama tele wameomba msamaha.

Wawili hao waliletwa pamoja na mjasiriamali mashuhuri Simon Kabu siku ya Alhamisi na wakawa na maafikiano mazuri.

Omondi na Maribe wamekiri kwamba walifanya  kosa kubw kuvuruta mtoto kwenye ugomvi wao na kumuweka kwenye faragha.

"Mimi na Jackie tumepelekana. Tunaomba msamaha. Tulikosea" Eric Omondi alisema.

Video ya wawili hao wakiwa  wamekumbatiana vizuri  huku wakisikiza ushauri kutoka wa Kabu imesambazwa sana mitandaoni.

"Sio nyinyi pekee mmekosa kusikizana. Mnaweza hisi mlifanya jambo mbaya, na kweli mlifanya. Lakini watu hukosana. Shoka zilizo kwa kikapu kimoja hugongana" Kabu aliwashauri Maribe na Omondi.

Wawili wao walikubaliana kwamba mtoto ni wao wote na kuahidi kuwa wako tayari  kushirikiana katika ulezi.

Hapo awali alasiri ya Alhamisi Omondi akiwa kwenye mahojiano katika Jalango TV aliomba Wakenya msamaha kwa niaba yake na Maribe.

"Nataka kuomba Wakenya msamaha  kwa niaba yangu na Jackie. Tulichofanya ni makosa sana. Tuliweka mtoto asiye na hatia kwa umma. Hakuna sababu ya kufanya vile" Omondi alisema.

Mchekeshaji huyo alikiri kwamba alikuwa amejuta matendo yake ila akaeleza kuwa alilazimika kuchukua hatua ile kuokoa jina lake.

"Nisingefanya hivo mambo yangeharibika. Nililazimika kusema ukweli wangu" Omondi alisema.

Omondi aliweka wazi kuwa hayuko kwenye mahusiano na Maribe kwa sasa na kudai kwamba huwa hawapatani mara kwa mara.