Kuwa 'single mother' sio ulemavu,' Akothee awashauri akina mama

Muhtasari
  • Akothee aghadhabishwa na akina mama wasiowajibikia watoto wao
akoth stylish 1 (1)
akoth stylish 1 (1)

Esther Akoth kama anavyojiita 'president of single mothers' amewashauri akina mama wawache drama za kufuatana na baba wa watoto wao.

Akothee ni miongoni mwa wasanii na wafanyibiashara wa kupiiwa mfano na wengi, haswa katika sekta ya kuwalea watoto peke yake.

Pia Akothee kweye ujumbe wake alisema kwamba ni mwanamke ambaye hana siri maishani mwake.

"Baby mama's wacheni! Single mothers wananitumia jumbe na kuniambia nifiche utambulisho wao, unanifahamu kweli? Unajua kuwa mimi ni mwanamke mmoja ambaye sina siri?

Una uhakika hata na hiyo story unayoniambia au ni simulizi kichwani🙆

Haloo Single mothers Halooooo Kuwa single mother sio ulemavu wala hadhi ni stori sasa ukinifuata mimi kama rais wako fuata nyayo zangu puuza maigizo ya baba mtoto ruhusu akina baba waone watoto wao kwani huwezi jipa ujauzito, Ruhusu baba mtoto aendelee na awe na maisha pia.

Huwezi kusababisha drama  katika maisha yako ya zamani Acha kumtumia mtoto kama silaha ili kupata mawazo yake, wewe kama mama unaharibu maisha ya mtoto wako ," Aliandika Akothee.

Akothee alikumbuka jinsi alimsaidia mama mmoja, na kuishia kunywa pombe na karo ya mwanawe.

"Hivi karibuni mtoto atakua, na atatembea huku na huko akimtafuta mtu yuleyule uliyemwambia amekufa!

Uwe mwanamke wa nguvu na usimamie maisha yako na ya mtoto wako 💪 Sitaburudisha upuuzi wa nyie kuwafunga wanaume na watoto wachanga kisha njooni kulia kwenye DM yangu, mimi pia sina suluhu kwenu

Nimekutana na akina mama wengi wasio na uwajibikaji, wengine waliwaacha watoto wao na wazazi wao wenyewe, na wanaweza kuniambia kwa furaha kuwa wanateseka 🤔

Nimejaribu kusomesha watoto wa single mothers,mmoja akiwa na watoto watatu aliishia kunywa karo ya shule nilimpeleka kwa watoto wake,nilipo tu kufika shule na watoto hawakuandikishwa shule moja,walikuwa nyumbani. kwa mwaka ."

Msanii huyo alidai kwamba akina mama ambao hawawajibikii watoto wao wanapaswa kukamatwa.