"Nimemiss jasho lako hebu njoo!" Nyota Ndogo amsihi mumewe arejee nchini mwezi mmoja tu baada ya kuondoka

Muhtasari

•Nyota Ndogo anaonekana karidhika sana kipindi ambacho mzungu huyo alikuwa hapa nchini kwani tayari anamuomba arejee tena.

•Wapenzi hao walijiburudisha na kuwa na wakati mwema pamoja kwa siku kadhaa ambazo Nielsen alikuwa hapa nchini huku wakizuru maeneo mbalimbali ya Kenya katika kipindi hicho.

Image: INSTAGRAM// NYOTA NDOGO

Takriban mwezi mmoja tu baada ya mume wa Nyota Ndogo,Henning Nielsen  kuondoka nchini baada ya kumtembelea kwa siku kadhaa, mwanamuziki huyo tayari anampeza tena Mdenmarki huyo.

Mwanamuziki huyo kutoka Pwani alionekana mwenye bashasha alipokuwa anamlaki mpenzi wake nchini mwishoni wa mwezi Septemba.

"Nikasema nimempeza, akaleta mwenyewe. Mapenzi ni kitu kingine usicheze na mapenzi" Nyota Ndogo alitangaza kuwasili kwa kipenzi chake kupitia ukurasa wa Instagram.

Wapenzi hao walijiburudisha na kuwa na wakati mwema pamoja kwa siku kadhaa ambazo Nielsen alikuwa hapa nchini huku wakizuru maeneo mbalimbali ya Kenya katika kipindi hicho.

Nyota Ndogo anaonekana karidhika sana kipindi ambacho mzungu huyo alikuwa hapa nchini kwani tayari anamuomba arejee tena.

"Nimemiss jasho lako hebu njoo" Msanii huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha iliyoonyesha akitazamana na mumewe uso kwa uso huku wakiwa na tabasamu kubwa kwenye nyuso zao.

Bwana Nielsen alipokuwa nchini alimtunuku mwanamuziki huyo na gari aina ya BMW kama  poza kwa kuumiza moyo wake alipokuwa amemtema na kumnyamazia mapema mwaka huu.

Msanii huyo alikuwa ameomba mumewe amnunulie gari ambalo alisema angetumia kufanya ziara zake za muziki na kuhudumia wateja wa biashara yake ya vyakula ya  @nyotandogo_jikoni.