logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini watu wanakonda?Msanii KRG amkejeli mkewe siku chache baada yake kudai hana nguvu za kiume

Kulingana na KRG, alijaribu kadiri alivyoweza kuokoa ndoa hiyo lakini yote yalikuwa bure.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri12 November 2021 - 18:42

Muhtasari


  • Kulingana na KRG, alijaribu kadiri alivyoweza kuokoa ndoa hiyo lakini yote yalikuwa bure
  • Alisema kuwa Lina hangebadilika na hakuna njia ambayo wanaweza kutengeneza familia nzuri.
  • Inavyoonekana, wawili hao bado 'wanapigana' na wanatumia kurasa zao za Instagram kutukanana

Mapema mwezi uliopita, msanii chipukizi KRG the Don alifichua kwambaanampa mkewe talaka rasmi  kwa sababu tu amekuwa akijihusisha na vitendo vya uasherati nyuma yake.

Kulingana na KRG, alijaribu kadiri alivyoweza kuokoa ndoa hiyo lakini yote yalikuwa bure.

Alisema kuwa Lina hangebadilika na hakuna njia ambayo wanaweza kutengeneza familia nzuri. 

Inavyoonekana, wawili hao bado 'wanapigana' na wanatumia kurasa zao za Instagram kutukanana.

Siku chache zilizopita, Lina aliacha post nyeti kwenye Instagram akisema kuwa 'mtu anataka umlelee watoto na kumbe hajui nguvu za kiume'.

Kwa kweli, ujumbe huo ulikuwa ukielekezwa moja kwa moja kwa KRG na leo, aliamua kujibu.

KRG alishinda kwa nini mkewe anazidi kukonda, huku akiuliza kama atakua hai mwishoni mwa mwaka huu.

"kwa nini watu wanakonda hivi? na mwezi haijaisha, chakula ndio shida au ni kumeza ndio shida,je?baada ya mwaka tutakua bado tupo au watu watakuwa wamejitia vitanzi,"Aliandika KRG.

Pia msanii huyo alishindwa kwa nini watu wanakasirika baada ya kuuliza swali hilo au kumkejeli mkewe, ilhali rafiki zake ndio wanamkejeli zaidi.

"Kwa nini watu wanakasirika?nilikuwa nasema kwa maana marafiki zake ndio walinitumia picha,za shosh ati anakula ngumu na kuvalia viatu vikubwa sana

Mara amekonda na mashavu yamekusha, kwa hivyo niliamua kuandika hapa ili atie bidii ya kumeza chakula wawache kuona hizo vitu negative."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved